"Baby daddy sumu!" Akothee aonyesha waziwazi kinyongo na baba wa mwanawe

Papa Ojwang ni mzungu kutoka Uswizi ambaye ni baba wa mtoto wa nne wa Akothee.

Muhtasari

•Akothee amekuwa akionyesha waziwazi uhasama wake mkubwa na baby daddy wake wa pili, Papa Ojwang.

•Alifichua kwamba kwa kweli  hakutaka kukutana na baby daddy huyo lakini alilazimika kwaNI alifaa kuwachukua wanawe.

•Akothee  alifichua kuwa alilazimika kurudi Kenya kutoka Uswizi baada ya Papa Ojwang kumfukuza takriban miaka kumi na minne iliyopita.

Akothee na baby daddy wake mzungu
Image: HISANI

Kwa kipindi kirefu mwimbaji mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee amekuwa akionyesha waziwazi uhasama wake mkubwa na baby daddy wake wa pili, Papa Ojwang.

Papa Ojwang ni mzungu kutoka Uswizi ambaye ni baba wa mtoto wa nne wa Akothee. Wawili hao walikuwa kwenye mahusiano takriban miaka kumi na minne iliyopita.

Katika mitandao ya kijamii, mama huyo wa watoto watano mara nyingi amemtaja Mswizi huyo kama 'Baby daddy sumu.'

Alitoa kauli kama hayo Alhamisi alipokuwa akienda kuwachukua wanawe wawili wadogo kutoka kwa mpenzi huyo wake wa zamani. 

"Hisia unayopata wakati unapaswa kukutana na baba mtoto mwenye sumu," Akothee aliandika chini ya video iliyoonyesha akiwa safarini.

Aliongeza, "Tunakutana kwa train station ya Basel ,ananipatie watoto ,napelekea yule mwingine anatungoja paris 🤦🤣🤣🤣 Ndani ya maisha ya Akothees, Usijaribu hii nyumbani."

Katika chapisho lingine, mwanamuziki huyo mwenye utata alifichua kwamba kwa kweli  hakutaka kukutana na baby daddy huyo lakini alilazimika kwa kuwa alifaa kuwachukua wanawe kutoka kwake.

Pia alifichua kuwa awali kulikuwa na mvutano kati yake na Papa Ojwang kuhusu jinsi ambavyo wangegawana muda wa kukaa na vijana hao.

"Sote tulikuwa tumepanga jinsi tunavyogawanya likizo ili sisi sote watatu (Baba na Mimi) tunapata kufurahia  muda na watoto wakati wa kiangazi. Wakati wangu na watoto ulikuwa umechanganyikiwa na kambi nyingi walizokuwa nazo na ziara zisizo na mpangilio nilizokuwa nazo ikanilazimu kufuta nyingi ili kuwa na watoto wangu 🤔 Sasa nikirudi kuomba papa kwa muda na watoto kwani nilikuwa na muda wote ikawa vita, Kwa kadri nilivyokuja huku nikiwa nimekunja mkia, niliomba tu ,niliomba kwa hisani 🙏 Nilimuomba bwana huyu aniruhusu nipate watoto kwa siku mbili au 3 tu ndani ya wiki zake mbili kwani Bern na Basel ni saa safari ya saa moja tu 🤦 ,Buda alikataa na kusema wasubiri kuanzia tarehe 18 sasa ni wakati wangu 🤔.

Unaweza kuwa nao kuanzia tarehe 18 watakaporudi Ufaransa 😭. Ooh iliniumiza vibaya. Nililia kwa masaa machache , nikajikusanya na kuangazia likizo zangu., hata mkinitukana sikuchaguana Kenya, Mimi huku nimeshikwa na mak*nde kama ziko. Kushughulikia baadhi ya Simba katika baadhi ya mashimo. Sikuweza kurudi Kenya kabla ya wakati bila kukaa na watoto wangu, hata hivyo sina deni la mtu yeyote maelezo wala kuomba msamaha. Nina maisha magumu mbali na kamera, kwa sababu mimi ni mwanamke mgumu anayeshughulika na mambo magumu. Inabidi nishughulikie na kurekebisha 💪," Alisema.

Mama huyo wa watoto watano alieleza furaha yake kubwa kukutana na wanawe na kupata nafasi ya kuwa nao. 

Baadae alipakia video iliyoonyesha akiwa na Ojwang', Oyoo pamoja na baby daddy wake wa mwisho Papa Ojwang'.

Mwanamuziki huyo hafichi kamwe mapenzi yake makubwa kwa baby daddy huyo wake Mfaransa ambaye bila shaka ndiye anayependelea zaidi.

Ni mara nyingi ambapo amemminia sifa kochokocho na hata kuonekana naye pamoja licha ya kutengana kwa miaka kadhaa iliyopita.

Mwezi jana, Akothee  alifichua kuwa alilazimika kurudi Kenya kutoka Uswizi baada ya Papa Ojwang kumfukuza takriban miaka kumi na minne iliyopita.

Alisema alikuwa na ujauzito wa miezi tisa wakati baba ya mtoto wake wa nne alipomfukuza. Wakati huo, Papa Ojwang alidai kuwa hakuwa tayari kuwa na mke ndiposa akamfukuza.

"'Rudi Afrika sina nguvu wala familia ya kutunza mwanamke mjamzito, siko tayari hata kuwa na mke' alisema baba mtoto wangu 👏💪," Akothee alisimulia kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 alikiri kuwa alipatwa na mawazo ya kujitoa uhai baada ya kupigwa teke na baby daddy huyo wake.

Nilifikiria kujitupa kwenye treni zinazopita, watoto wangu walikuwa wakinipigia simu mara kwa mara nchini Kenya, haswa Vesha, nilikaa kwenye baridi huko Basel BBB wakati wa msimu wa baridi mwezi Februari kwa usahihi 🙆‍♂️ mikahawa yote ilikuwa imefungwa na nilikuwa karibu kuachwa peke yangu, kwa wale wa Ulaya wanajua inavyojisikia kwenye vituo vya treni masaa ya usiku wakati treni zinafungwa," Alisimulia.

Pia alieleza kuwa kufukuzwa kwake na mumewe huyo wa zamani kulifanya asitamani tena kuishi Ulaya.

"Sitamani chochote, nakuja hapa kufanya mambo yangu na kurudi AFRICAAAAA," Alisema.