Meneja wa Diamond, Sallam SK afunguka kuhusu kumtema na kufanya kazi na Harmonize

Sallam alibainisha kuwa kujiunga na Kondegang itakuwa ni kujidhalilisha.

Muhtasari

•Sallam SK Mendez amefutilia mbali uwezekano wa yeye kujiunga na lebo ya Harmonize ya Konde Music Worldwide.

•Mendez pia alidokeza kuwa bado  hajaondoka kwenye lebo ya WCB.

Diamond Platnumz na meneja wake EL-Jeffe Mendez
Diamond Platnumz na meneja wake EL-Jeffe Mendez
Image: INSTAGRAM// SALLAM SK

Meneja  wa Diamond Platnumz Sallam SK Mendez amefutilia mbali uwezekano wa yeye kujiunga na lebo ya Harmonize ya Konde Music Worldwide.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini Tanzania, alibainisha kuwa kujiunga na lebo ya Harmonize itakuwa  ni kujidhalilisha.

Mendez alidokeza kuwa analenga zaidi kuenda kimataifa baada ya kuondoka Wasafi na hana mpango wa kurudi nyuma.

"Kwa kweli mtakuwa mnanikosea adabu kusema eti mimi nitoke Wasafi niende Konde. Wakati ambapo ninaweza kufanya naye kazi ni aidha arudi Wasafi au nifungue lebo aje ajiunge na lebo yangu. Nitakuwa nimeshuka daraja!" alisema.

Mendez pia alidokeza kuwa bado  hajaondoka kwenye lebo ya WCB, kinyume na tetesi ambazo zimekuwepo kuwa alitengana na Diamond.

Tetesi kuwa meneja huyo amemuaga Diamond na anapanga kuungana na Harmonize zilianza kuvuma baada ya kuonekana wakikumbatiana na bosi huyo wa Kondegang wakati wa moja ya tamasha zake ambayo lilifanyika Zanzibar.

Mendez hata hivyo amefichua kuwa msanii huyo wa zamani wa WCB ndiye aliyemualika katika tamasha hiyo akitaka wamalize tofauti zao.

"Kwa sababu alikuwa ameonyesha nia ya kutaka kuyamaliza kati yetu na tumepata nafasi ya kuonana naye niliona sina tatizo naye," alisema.

Hata hivyo alidokeza kuwa yeye, Diamond na Babu Tale hawana beef naye. Alisema kuwa Harmonize ndiye anayepigana nao

Katika siku za hivi majuzi kumekuwa na tetesi  kwamba Sallam SK aliacha kufanya kazi na Diamond miezi michache iliyopita.

Mashabiki waligundua kuwa meneja huyo haandamani tena na Diamond Platnumz kwenye ziara zake kama ilivyokuwa awali.

Hatua ya Sallam kuhudhuria moja ya shoo za Harmonize ilizidisha tetesi hizo huku ikidaiwa wanapanga kufanya kazi pamoja.