DJ Lisney ajitosa kwenye siasa, kuwania ubunge Dagoretti Kaskazini

Muhtasari

• Ushindani mkali unatarajiwa kuonekana baina ya LAisney na Jahmby Koikai ambao wote ni watu mashuhuri katika tasnia ya muziki na ambao wametangaza kuwania ubunge Dagoretti Kaskazini

• Ushindani mkali unatarajiwa kuonekana baina ya LAisney na Jahmby Koikai ambao wote ni watu mashuhuri katika tasnia ya muziki na ambao wametangaza kuwania ubunge Dagoretti Kaskazini

DJ Lisney
Image: Facebook

DJ Lisney ameingia katika orodha ya watu ambao wametangaza kuwania nyadhifa mbali mbali za kisiasa katika uchaguzi mkuu mwezi Agosti.

Kama wenzake wengi walioweka azma ya kuwakilisha watu kwa nyadhifa mbalimbali za kisiasa nchini, bango la Lesney linaonyesha wazi kuwa yupo tayari kuwakilisha watu wa Dagoretti Kaskazini bungeni kama mbunge huru asiye egemea chama chochote cha kisiasa.

Akiweka tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram, Lisney ameweka bango hilo na kufuatisha na ujumbe,

“Wakati wa mabadiliko”

DJ Lisney
Image: Instagram

Dj Lisney ambaye jina lake kamili ni Linda Felix amejiunga kwenye orodha ndefu ya wasanii na watu mashuhuri kujitosa katika siasa wakiwemo Dorea Chege, Ruffton, Stacy Ndaisi, Jamal Gaddafi, Jalang’oo, Jahmby Koikai miongoni mwa wengine.

Ushindani mkali unatarajiwa kuonekana baina ya LAisney na Jahmby Koikai ambao wote ni watu mashuhuri katika tasnia ya muziki na ambao wametangaza kuwania ubunge Dagoretti Kaskazini

Mashabiki wa mcheza santuri huyo wamempa hongera kwa ujasiri wake wa kutaka kuwakilisha watu wa Dagoretti Kaskazini