Valentino ina mambo! Nicah amuosha mumewe miguu

Muhtasari

• Msanii wa injili Nicah the Queen amezua mawazo mseto mitandaoni baada ya kupakia mkanda wa video akimuosha mume wake miguu.

• Nicah alikuwa ameolewa na mcheshi kutoka Nigeria, Dr Ofweneke

Nicah the Queen
Image: Instagram

Msanii wa injili Nicah the Queen amezua mawazo mseto mitandaoni baada ya kupakia mkanda wa video akimuosha mume wake miguu.

Katika video hiyo, Nicah anaonekana akimsugua mumewe miguu kwa sabuni  huku akiifuatisha na maneno,

“Mwanamke penda hadi wakome dah! Slahver baba eeeh wafaidi.”

Hii ni video ya pili baada ya kupakia video nyingine na muwe huyo juzi akisema kwamba huyo naye akimuacha basi atamuandikia albamu nzima ya muziki,

“Huyu namwandikia album akiniwacha ama nimuwache inaitwa zilizopendwa!!Kudate msanii rahaa!! Eeeh baba eeeh Slahver wafaidii.” Aliandika Nicah

Image: INSTAGRAM

Ikumbukwe msanii Nicah alikuwa ameolewa na mcheshi kutoka Nigeria ambaye makao yake ni nchini Kenya, nazungumzia Dr. Ofweneke lakini wakaachana miaka michache iliyopita.

Nicah alisadiki kwamba hakuwahi mfanyia Ofweke vitu kama hivyo alivyokuwa akimfanyia mwanaume wake wa sasa.

Lakini baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wamezua maoni mesto huku wengine wakisema kwamba anafanya hivo kwa sababu siku ya wapendanao inakaribia.

“14 imekaribia, tunawajua sasa mnaweza fanya kila kituili msiachwe siku ya valentino,” mmoja wa mashabiki wake aliandika.