Bobi Wine asherehekewa na mkewe siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari

• Aliyekuwa mwanamuziki na mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine ni mwanamme mwenye furaha.

• Wewe ni mahali pangu pa kupumzikia na kama mimi ni kitu chochote basi mimi ni wako. Heri njema ya siku ya Valentino,” ameandika Barbie kwenye Instagram yake

Bobi Wine na familia yake
Image: HISANI

Aliyekuwa mwanamuziki na mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine ni mwanamme mwenye furaha.

Haya ni baada ya mkewe Barbie Kyagulanyi kumlimbikizia sifa sufufu siku hii ya wapendanao, siku chache baada ya Bobi kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kufika miaka 40.

Barbie Kyagulanyi amemlimbikizia sifa Bobi na kusema kwamba uamuzi pekee aliofanya wa kweli ni kuolewa na mwanasiasa huyo ambaye anapendelewa sana na  raia wengi nchini Uganda.

“Sijui ni kwa nini tena sihangaiki kabisa na kulewa kwa kukupumulia tu. Wewe ni manukato ninayopenda Zaidi, bustani yangu ya waridi jekundu na nyuki wanaonguruma ndani mule. Wewe ni upepo mwanana wa alfajiri ya saa kumi na moja, mwezi wangu kamili ukiangaza juu ya maji ya ziwa tulivu. Wewe ni mahali pangu pa kupumzikia na kama mimi ni kitu chochote basi mimi ni wako. Heri njema ya siku ya Valentino,” ameandika Barbie kwenye Instagram yake.

Kwa upande wake Bobi Wine amemsherehekea mkewe kwa ujumbe mtamu na kusema kwamba anampenda kwa niaba ya mababu wote.

“Barbie Kyagulanyi mpenzi wangu, nakupenda kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya mababu zangu wote na vizazi vyangu pia. Wewe ni jambo bora kuwahi kutokea kwangu na unajua hilo,” amemsifia Bobi.