2Mbili amuingilia DJ Shiti kwa kutoa 150 pekee kwa malezi ya mtoto

Muhtasari

• 2mbili atoa parody ya kumchqamba DJ Shiti kwa kutoa 150 pekee kwa malezi ya mwanawe.

2mbili
Image: Instagram

Mchekeshaji 2mbili amemuingilia mchekeshaji mwenza DJ Shiti kwa kile alikitaja kwamba ni aibu kwa msanii mkubwa kama Shiti kutumia aliyekuwa mkewe Fash shilingi 150 za Kenya kwa malezi ya mwanawe Miriam.

2Mbili amefanya parody ya ngoma ya Diamond Platnumz, Gidi na kupachika maneno ya kumuapisha Shiti kwamba ni aibu kutoa shilingi mia hamsini pekee na kujigamba kama mwanaume kwamba anashughulikia malezi ya mwanawe.

 “Shiti huna akili, yaani 150. Shiti you are very silly, me nafeel kukupiga head mpaka down. Na vile unabrag eti wewe una money, na kama umesota si urudi nyumbani,” kipengee kimoja cha parody hiyo kinasema.

2Mbili amezidi kumchamba Shiti na kumuambia aache mchezo na afanye maamuzi ya maana kutuma pesa za maana ili mtoto akule kwa sababu Shiti anajishauwa kwamba ana pesa haswa baada ya kuangukia dili la kuwa balozi wa kampuni ya ubashiri ya SportPesa.

“Wacha mchezo tuma pesa mtoto akule, punguza moto pia mafegi pesa zako utume kule,” kipengele kingine kinasema.

Haya yanakuja siku chache tu baada ya aliyekuwa mkewe Shiti kudai kwamba anapitia msongo wa mawazo na amefikia uamuzi wa kumrudisha mtoto kwa babake kwa sababu mwenyewe ameshindwa na kumlea.

Mapema Shiti alijitetea kwamba yeye anajua hajawahi feli kushughulika malezi kamili ya mwanawe hata baada ya kutengana na mkewe lakini baadae Fash akafichua kwamba hela hizo anazodai ni za kushughulikia mtoto ni kiasi kidogo sana na mpaka akakitaja kuwa 150 za shilingi za Kenya.