Eddie Butita: Niko bize lakini nikiitwa Young Famous & African nitaenda

Muhtasari

• Eddie Butita amewashukuru wakenya ambao wanalitaja jina lake kama mtu ambaye ana uwezo wa kushiriki katika kipindi cha Netflix cha Young Famous and African.

• "Asante kwa kuniamini. Sichukulii kuwa umeniamini sana, kwa sasa niko busy lakini wakinifikia, nitatenga muda kidogo ili nijiunge nao," alisema Butita

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Eddie Butita

Mchekeshaji na muongozaji wa video Eddie Butita ameweka wazi kwamba hata inagwa kwa sasa yuko bize, lakini nafasi ikijipa ya kuitwa ili kujumuishwa katika kipindi cha uhalisia cha Young, Famous and African kwenye Netflix, bila shaka atajiunga.

Butita pia amewashukuru Wakenya na watu wote ambao wamekuwa wakilitaja jina lake katika mijadala ya mitandaoni ambamo watu walikuwa wanauliza maoni kuhusu Mkenya yupi anaweza liwakilisha taifa katika kipindi hicho nafasi ikijipa.

“Nimepokea DM nyingi, Simu na Barua pepe nyingi ambazo ilibidi nizime kabisa simu yangu Jana. Watu wengi wanasema niwe kwenye Young, Famous na African. Asante kwa kuniamini. Sichukulii kuwa umeniamini sana, kwa sasa niko busy lakini wakinifikia, nitatenga muda kidogo ili nijiunge nao.” Aliandika Butita kwenye Instagram yake.

Wakenya wengi wameshabikia kipindi hicho ambacho kimewashirikisha Diamond Platnumz kutoka Tanzania na Zari Hassan kutoka Uganda miongoni mwa mastaa wengine maarufu.

Lakini Wakenya walionekana kutofurahia suala kwamba hakuna Mkenya hata mmoja ambaye alichaguliwa kuwakilisha Kenya ambapo walianzisha mijadala mitandaoni kuwataja wale ambao wanaona wana uwezo wa kujumuishwa.

Baadhi walimtaja mrithi wa kampuni ya vileo ya Keroche, Anerlisa Muigai ambaye baadae alifichua kwamba alipata mwaliko lakini akaukataa.

Mtangazaji Betty Kyallo, mchekeshaji Eric Omondi ni baadhi pia ya majina ambayo yalitajwa kuwa Wakenya wenye umri mdogo na ambao wana umaarufu mkubwa na ufanisi maridhawa katika kazi zao.