"Sikumbuki tukiwa marafiki," Amber Ray afunguka kuhusu madai ya ugomvi na Vera Sidika

Muhtasari

•Amber Ray amefichua kuwa hakujawahi kutokea uhusiano wowote wa karibu kati yake na Vera ambao uligeuka kuwa uadui.  

•Wanasoshalaiti hao wawili wamedhaniwa kutokuwa na uhusiano mwema tangu Vera alipojitosa kwenye mahusiano na mpenzi wa zamani wa Amber Ray, Brown Mauzo.

Amber Ray na Vera Sidika
Amber Ray na Vera Sidika
Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray amefunguka kuhusu madai ya kuwa na ugomvi na mwenzake Vera Sidika.

Akizungumza kwenye ukurasa wake wa Instagram, Amber Ray aliweka wazi kwamba hakuna uhasama wowote kati yake na mke huyo wa Brown Mauzo.

Mwanasoshalaiti huyo amefichua kuwa hakujawahi kutokea uhusiano wowote wa karibu kati yake na Vera ambao uligeuka kuwa uadui.  

"Sikumbuki tukiwa marafiki. Tuliacha lini kuwa marafiki?" Amber Ray alimjibu shabiki aliyemuomba akubali kusameheana na Vera.

Haya yanajiri takriban wiki mbili baada ya Vera kuweka kukiri kuwa hana beef yoyote na mpenzi huyo wa zamani wa Brown Mauzo.

"Ukweli ni kuwa sina ugomvi na mtu yeyote. Mimi ni mtu wa kupenda kila wakati." Vera alijibu alipouulizwa kuhusu ugomvi wake na Amber Ray.

Wanasoshalaiti hao wawili wamedhaniwa kutokuwa na uhusiano mwema tangu Vera alipojitosa kwenye mahusiano na mpenzi wa zamani wa Amber Ray, Brown Mauzo.