"Harmonize akijikuna kwapa na kuweka YuoTube atapata views +1M, ni msanii mkubwa" - Mwijaku

Muhtasari

• Mwijaku - "Harmonize ni msanii mkubwa hata akisema ajikune kwapa lake na aweke YouTube atapata views zaidi ya milioni kwa dakika,”

Harmonize, mwijaku
Harmonize, mwijaku
Image: INSTAGRAM///MWIJAKU

Mtangazaji wa kituo cha habari cha Clouds kinachopimana ubabe na kituo cha msanii Diamond cha Wasafi, Mwijaku amemtetea msanii Harmonize kuhusu madai ya kughushi views kwenye mtandao wa YouTube kwa collabo yake na Ibraah ya Mdomo.

Collabo hiyo iliandikisha rekodi ya kushtua ambayo kama ungelikuwepo uwezo basi moja kwa moja ingeingia kwenye kitabu maarufu duniani cha Guinness Book of Record.

Ngoma hiyo iliandikisha rekodi zisizoaminika katika upeo wa fikira za wanadamu kwani chini ya dakika tatu tu tayari watu zaidi ya milioni 1.3 walikuwa tayari washaitazama, hata kabla ya ngoma yenyewe kukamilika, kwa sababu urefu wa ngoma ni dakika 3 na sekunde 17.

Cha kushangaza zaidi na ambacho kilifanya watu waamini kabisa kuwepo na hali ya kughushi au kubuni views, ngoma hiyo kwa zaidi ya saa 10 baadae, ilishindwa kabisa kupiga hatua kwa kasi ile ile iliyoanza nayo, kwani ilikwama kwa views milioni 1.4 tu, maana kwamba ilifanikiwa kupata watazamaji zaidi ya milioni chini ya dakika lakini ikashindwa kuzidi watazamaji laki katika saa kadhaa.

Mwijaku ambaye siku zote anapinga wasanii kutoka Wasafi na kuwapendelea wasanii mahasidi wa Wasafi amejitoa wazi na kusema kwamba hakuna ja kununua views pale kwani Harmonize ni msanii mkubwa na ana uwezo wa kufika views zaidi ya milioni kwa haraka hata akijikuna kwapa na kupakia kwenye YouTube.

“Kama kuweka ROBOT ni rahisi basi na nyinyi wekeni. Harmonize ni msanii mkubwa hata akisema ajikune kwapa lake na aweke YouTube atapata views zaidi ya milioni kwa dakika,” Mwijaku alimtetea.