Sijakaliwa!Mke wangu lazima ajue kila kitu -Mwijaku

Muhtasari

• Mwijaku amesema kwamba lazima amfahamishe mke wake chochote anachokisema kwenye vyombo vya habari.

• Alisema kwamba ndo sababu iliyofanya ndoa yake kudumu kwa muda mrefu.


Mwanahabari wa Clouds fm huko Tanzania, Mwijaku amesema kwamba lazima amfahamishe mkewe kuhusu chochote anachokizungumza katika mahojiano na vyombo vya habari mbalimbali.

Akizungumza na mwanablogu wa Global tv online, Mwijaku alisema kwamba mke wake humpa ushauri kuhusu chochote anachopanga kuzungumza.

"...Mimi lazima nimwambie mke wangu yote ninayoyazungumza kwenye mahojiano. Ananishauri sana nifuate sheria ninapozungumza," Mwijaku alisema.

Alidokeza kwamba mke wake sio mtumizi wa mitandao ya kijamii hivyo lazima amfahamishe chochote anachokifanya kwenye mitandao ili kujenga mazingira ya uwazi kati yao.

Mwijaku ni moja kati ya mastaa wa Bongo ambao wameweka wazi mahusiano yao na mara kwa mara ameshuhudiwa akimsifia mke wake.

Alitoa wosia kwa chipukizi wote wanaoingia kwenye ndoa kuwa wakweli kwa wapenzi wao iwapo wanataka ndoa zao kudumu.