"Adui ni umaskini na Arsenal" Femi One asema alipoona picha ya zamani ya Terence Creative

Terence alipakia picha yake ya zamani akisema alikuwa mwandishi wa riwaya.

Muhtasari

• “Waaah watu hutoka mbali kweli. Papa Freddy hapo ulikuwa mashambani hakukuwa na biashara huko?” shabiki mwingine alistaajabu kwa picha hiyo

Mchekeshaji na muigizaji huyo alisema aliwahi kuandika riwaya
TERENCE CREATIVE Mchekeshaji na muigizaji huyo alisema aliwahi kuandika riwaya
Image: Instagram//Terence creative

Mchekeshaji Terence Creative ambaye jina lake halisi ni Lawrence Mwangi Macharia amepakia picha yake ya zamani kabla ya utajiri na umaarufu na kusema kwamba katika maisha, hakuna kitu ambacho hajawahi jaribu.

Muigizaji huyo aliyepata umaarufu mkubwa kupitia vipindi vyake vya kuigiza kama Mkongo tapeli kwa jina Papa Fred Ngamwaya alionekana kweney picha hiyo akiwa ameshikilia kitabu aina ya riwaya ambacho alidai ni chake alichokiandika mwenyewe.

“Ila kitambo nilikuwa nimeandika kitabu, haya maisha hakuna kitu sijajaribu mimi,” Terence aliandika kwenye picha hiyo.

Katika picha hiyo, Terence anaonekana kudhoofika kweli huku amechakaa mwanzo mwisho kinyume na anavyokatiza siku hizi kwa fasheni za aina yake na watu wengi waliofurika kuachia maoni yao walisema kweli maisha ni safari ndefu sana.

“Adui ni umasikini na Arsenal,” aliandika mwanamuziki wa kufoka Femi One.

“Wueh, Mungu anaponya,” msanii wa Injili Hopekid alisema.

“Waaah watu hutoka mbali kweli. Papa Freddy hapo ulikuwa mashambani hakukuwa na biashara huko?” shabiki mwingine alistaajabu kwa picha hiyo ambayo kwa yule hajamzoea Terence kwa ukaribu unaweza ukasema ni watu wawili tofauti kabisa kama mwanga na kiza.

Siku yake ilipofika, Terence alifanya ‘skit’ ya kuchekesha tu kama kawaida lakini ikapata mapokezi makubwa kutoka kwa wakenya walioshabikia kwa weledi wake wa kuigiza lafudhi ya Kikongo katika kipindi hicho kwa jina Wash wash.

Kwa sasa, yeye ni balozi wa mauzo katika kampuni mbali mbali za humu nchini ambapo wamefungua biashara kadha tajika na mpenzi wake Milly Chebby ambaye juzi walisherehekea miaka 10 katika ndoa.