Usifananishe mapenzi na chakula - Rayvanny, ajuta kumpenda Paula

Msanii huyo alidhibitisha kwamba alifanya jambo la maana kubwa kukatisha mahusiano yake na mrembo Paula Masanja.

Muhtasari

• Alitoa ushauri huu baada ya kuweka wazi kwamba mahusiano yake na mrembo Paula hayapo tena.

• Wiki jana alidokeza kwa video kurudiana na mpenzi wake Fahyvanny ambaye ni mzazi mwenzake.

Rayvanny ajuta kumpenda Paula
Rayvanny ajuta kumpenda Paula
Image: Maktaba

Bosi wa lebo ya Next Level Music Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny hatimaye ameweka wazi kwamba yeye na Paula Kajala hawapo tena pamoja.

Kupitia Instagram yake, Rayvanny alisema kwamba jambo hilo lilikuwa linamnyima amani ya nafsi ya akili na aliamua kuchukua uamuzi mgumu na kisha kuanza safari ya matumaini – Kuvunja mahusiano yake na binti huyo wa kambo wa msanii Harmonize.

Staa huyo alichukua pia fursa hiyo kuwashauri watu kutofanya mfananisho wa mapenzi na chakula kwani ni vitu viwili tofuati.

Rayvanny amabye ni baba wa mtoto mmoja miaka michache nyuma alimbwaga aliyekuwa mpenzi wake na mzazi Fahyvanny.

Kabla ya kuthibitisha kuachana na Paula Kajala, mwimbaji Rayvanny aliendelea kuzungumzia mapenzi akisema hakuna mtu anayepaswa kuwachanganya kutokana na kuona ukweli wa mambo. Aliendelea kuongeza kuwa baada ya miezi michache ya kupata ‘mapenzi’ hatimaye akapata amani na moyo wake na kuachana na uhusiano wake na Paula.

“Usiruhusu mapenzi yakuchanganye, usifananishe mapenzi na chakula, nilifanya amani na moyo wangu na kukatisha uhusiano wangu na Paula,” Rayvanny aliandika.

Ingawa hakuingia katika maelezo kuhusu kutengana kwa muda wote - kumwambia majuto yake inamaanisha tu kwamba alidhulumiwa na msichana huyo mbichi au hakuwahi kumpenda kama vile alivyotarajia.

Baadhi ya wale wanaofuatilia mahusiano yao wanakisia kwamba kutengana kwao au kufifia kwa mahusiano yao huenda kulitokana na mamake Paula, Fridah Kajala kurudiana na msanii Harmonize ambaye awali walitengana kwa sababu ya huyo Paula kuviziwa na Harmonize.

Paula hivi juzi alidhibitisha kumkubali Harmonize kama baba yake wa kambo na hata kumsifia hadharani kwamba anajua kucheza densi vizuri alipofanya klipu ndogo wakicheza na mamake.

Harmonize pia ameonekana kumsifia sana Paula kwa kumuita kama binti yake na hata kutangaza biashara yake ya nguo, Paula Closet kwa mashabiki wake.

Kando na hayo, pia wiki jana Rayvanny alidokeza kwa video kwamba huenda amerudiana na Fahyvanny baada ya kutengana kwa zaidi ya miaka mitatu, ambapo wamekuwa wakishirikiana kulea mwanao wakiwa kando kando.