Tangu King Kaka augue vibaya, nilijenga ukaribu wangu na Mungu - Nana Owiti

Watoto wangu walichanganyikiwa haswa waliponiona nikilia - Nana Owiti.

Muhtasari

Siwezi kuhesabu mara ambazo nilimpigia simu mchungaji wangu ili tu kuomba nami kupitia simu - Nana Owiti.

Nana Owiti asimulia alivyojenga ukaribuy na Mungu baada ya kuugua kwa mumewe King Kaka
Nana Owiti asimulia alivyojenga ukaribuy na Mungu baada ya kuugua kwa mumewe King Kaka
Image: instagram

Kwa wale mnaokumbuka vizuri, msanii maarufu nchini Kenya, King Kaka mwaka jana alikumbwa na matatizo ya kiafya ambayo yalimpelekea kulazwa na kupoteza uzito wa mwili wake kwa kasi mno.

Katika wimbo ambao aliuachia pindi baada ya kupona, msanii huyo alisimulia kwenye collabo yake na Nviiri, wimbo uliobatizwa kwa jina Manifest. King Kaka alieleza kuwa dakatari alimfanyia vipimo tofauti na kumuandikia dawa zisizofaa, jambo ambalo lilidhoofisha hata zaidi afya yake.

Mkewe, Nana Owito sasa amefunguka kwamba tangu tukio lile la kulazwa kwa mumewe, alijipata amejongea karibu sana na Mungu na kujenga uhusiano ambao haukuwepo hapo awali.

“Nitakuwa mkweli tangu King alipougua na kuponywa, nilipata mwamko wa kiroho. Nilihisi kuchanganyikiwa. Kama familia tulitikiswa sana ilipokuwa ikitokea na tulikuwa na sehemu moja tu ya kukimbilia na hiyo ilikuwa kwa Mungu!” Nana Owiti alisimulia.

Pia alifunguka kwamba alikuwa na mashaka mengi ambayo yalimfanya kumtafuta mchungaji wao mara kwa mara kwa ajili ya Imani ya kirogo na Maombi kwa mumewe. Jambo hilo liliwafanya hata watoto wake kuwa na wasiwasi kuhusu afya ya baba yao na kwa simulizi yake, Owiti alisema kilikuwa kipindi kimoja kigumu sana.

“Siwezi kuhesabu mara ambazo nilimpigia simu mchungaji wangu mpendwa, Pastor Njoro ili tu kuomba nami kupitia simu. Mara kadhaa ningempigia simu tu kumwambia sikuwa na nguvu tena na mume wangu alikuwa akielekea kuisha. Idadi ya mara ambazo yeye na mke wake walikuwa wakikimbia nyumbani hata usiku ili kusali pamoja nasi(Mungu! Watoto wangu walichanganyikiwa 😕haswa waliponiona nikilia 😢) Nisisahau kamwe jinsi nilivyohitaji mguso wa Mungu 😭Bado ninamhitaji,” Nana Owiti aliibua hisia.

Alisema kwamba kikubwa ambapo kilikuwa kikizunguka ndani ya kichwa chake ni kuomba tu mumewe apone na kurejelea hali yake ya kawaida. Na pia wasiwasi huo ulimfanya kuapa kwamba pindi mumewe atakapopona hivi basi atahakikisha hata watoto wake wamemjua Mungu kwa hali na mali.

“Mimi si mkamilifu kwa kweli mbali na hilo lakini uhusiano wangu na Mungu siku zote umekua💯 ..Pia, niliweka nadhiri kwamba watoto wangu wangejua Mungu ni nani. Wangemjua si tu mponyaji bali mrejeshaji wa uzima,” Mtangazaji huyo wa runinga aliandika huku akipakia picha yake na watoto wake pamoja na yaya baada ya kanisa.