Bahati ampongeza Diana kwa ujasiri aliouonyesha wakati wa upasuaji wa kujifungua

Bahati alimshukuru Diana kwa kubeba ujauzito wa mtoto wake.

Muhtasari

• Bahati alisema kuwa hawezi kumlinganisha mke wake kwa mwanamke yeyote yule duniani kwani Marua ni wa kipekee.

•Bahati alieleza jinsi alivyomthamini na kumheshimu kwa yote hayo.

Bahati na Diana Marua

Mwanamuziki Bahati amemwandikia mke wake, Diana Marua ujumbe mtamu wa kumshukuru baada ya kujifungua.

Kwenye Instagram, Bahati alimshukuru Marua kwa kuwa mzazi wa watoto wake na zaidi kuwa mama bora.

"Nimekupenda zaidi kwa kubeba ujauzito na kulea watoto wangu.... ILA Nimekuheshimu ZAIDI kwa kujiamini katika chumba cha upasuaji ulipopitia upasuaji  wa kumkaribisha Binti Yetu @MALAIKA_BAHATI," aliandika.

Alisema kuwa hawezi kumlinganisha mke wake na mwanamke yeyote yule duniani kwani Marua ni wa kipekee.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa alishuhudia jinsi mkewe alivyokuwa mtulivu wakati wa upasuaji wa kujifungua.

Alieleza jinsi alivyomthamini na kumheshimu kwa yote hayo.

"Kwa uhakika siwezi kukufananisha na mwanamke yeyote chini ya jua... Kwa sababu hakuna anayejua ulipitia nini ili niweze kuitwa baba tena!!! Hakika Wewe ni  Super Woman wangu, mama @MALAIKA_BAHATI ," mume huyo wa Marua alisema.

Alimshukuru Mungu kwa kufanikisha upasuaji wa Marua.

Siku ya Jumatano Wanandoa hao walitangaza kuzaliwa kwa binti yao Jumanne tarehe 1 wezi wa Novemba na kumpa jina Malakia Nyambura Bahati.

Wawili hao walipokea jumbe za heri njema mitandaoni kutoka kwa mashabiki wao wakiwemo watu mashuhuri.

Mashabiki wao wamekuwa wakionyesha dalili za kuchoshwa na habari za wanandoa hao za kujifungua kila kuchao.