Nameless aingiwa na kiwewe baada ya mvulana kusimama karibu na bintiye Tumiso

Nameless alipakia picha hiyo na kuzua utani kuwa alikuwa anafuatilia kwa ukaribu.

Muhtasari

• Watu walimfanyia mzaha Nameless huku wakisema kuwa uzazi ni kazi ngumu sana ambayo inahitaji mzazi kufuatilia wanawe muda wote bila likizo.

Nameless akiwafuatilia bintiye na kijana aliyesimama kando yake
Nameless akiwafuatilia bintiye na kijana aliyesimama kando yake
Image: instagram

Wikendi iliyopita msanii Nameless alikuwa na matembezi na binti yake kifungua mimba, Tumiso na alipakia picha ambapo binti yake alikuwa amesimama huku kijana wa kiume akionekana pia kando yake.

Katika picha hiyo, Nameless alionekana akijipitisha karibu na wawili hao huku akiibua gumzo la utani mitandaoni kwamba alikuwa anafanya hivyo makusudi tu kama baba anayemtakia binti yake mema kwa kutotaka kijana yeyote kumkaribia kwa njia hasi.

Kijana huyo alisimama bega kwa bega na Tumiso aliyevalia fulana ya pinki na suruali ya jeans iliyochanika. Ukaribu wa wawili hao ulionekana kumkosesha raha baba mabinti Nameless.

 Nameless aliwachekesha watumiaji wa mtandao baada ya kufichua kwamba alikuwa akiangalia kwa karibu hali hiyo huku akishangaa ni nini kilifanyika kwa hatua za kutengwa kwa jamii.

“Ufuatiliaji kwa karibu. Bega kwa bega kwa nini? Hii Ndio Kusugua Mabega Ama? Ni nini kilitokea kwa umbali wa kijamii, kusema kweli?” Nameless aliuliza kwa mzaha na utani.

Chapisho hili lilizua vichekesho kutoka kwa baadhi ya wanamitandao ambao walimtania kwamba anafaa kuacha watoto wajuane na wengine wakimtania kuwa anafaa kukubali ili aitwe babu mapema.

“Hutaki kuitwa guka na mapema ndio best?” Gracious Grace alimtania.

“Ninakubaliana na wewe, unaweza kuhitaji mbwa wachache wakali 🐕 karibu na kiwanja chako, uzuri huo ni mwingi, naweza kutoa ulinzi huo,” mwingine kwa jina Mbwaya aliandika.

“Hahahahahahahahaha uzazi ni kama kufanya kazi Scotland Yard au kitu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣na kuwa na aibu wakati huo huo hahahaha 😂😂😂😂😂,” Tabitha Atieno alisema.