Mapenzi bado ni tight!: Samidoh na Edday wafanyiana utani wa kimahaba mtandaoni

Edday alipakia chapisho la simulizi ya utotoni mwake na Samidoh akamjibu kwa utani kwamba anamjua kwa utundu wake.

Muhtasari

• Licha ya Edday kudokeza kwamba maji yamemfika kwenye koo katika ndoa hiyo ya miaka 15, hakuwahi weka wazi endapo ameamua kuachana na Samidoh.

• Lakini kwa jinsi walikuwa wanadekezana kwa mahaba, wengi wanahisi badi kuna mapenzi mazito baina yao.

Edday Nderitu na Samidoh wafanyiana utani wa kimahaba huku kukiwa na fununu kuwa wameachana.
Edday Nderitu na Samidoh wafanyiana utani wa kimahaba huku kukiwa na fununu kuwa wameachana.
Image: Facebook//Edday Nderitu

Samidoh na mke wake wa kwanza Edday Nderitu wamedhihirisha kwamba bado wanapendana pakubwa, licha ya msukosuko uliotishia kuyumbisha ndoa yao ya miaka 15 mwezi mmoja uliopita.

Samidoh aliweka maoni yake kwenye chapisho la Nderitu kwenye mtandao wa Facebook akidokeza kwamba anamjua vizuri tena kwa undani, akilenga kuzungumzia hadithi ya zamani ambayo mkewe wa kwanza Nderitu alikuwa anasimulia kwa wafuasi wake.

 Nderitu alikuwa anasimulia jinsi alidanganywa na rafiki yake wakati anaenda shule, rafiki huyo alimwita na kumtaka wasimame kando ya barabara ili kumsubiri rafiki mwingine, kumbe rafiki huyo wa kwanza hakuwa anaenda shule siku hiyo na alikuwa anataka kupana rafiki mwingine wa kukaa na yeye bila kwenda shule.

Katika simulizi hilo, Samidoh alijibu kwa utani kwamba anamjua vizuri sana si yeye aliitwa kando ya barabara bali ni yeye alikuwa hataki kwenda shule na ndiye alimwita rafiki yake.

“Na kwa vile nakujua vizuri nina uhakika ni wewe ulimuita upande wako!” Samidoh aliandika kwa utani.

Hata hivyo, Edday alimjibu kwa utani huo huo pia akisema kwamba anamjua yeye ni msichana mzuri na kumtaka kutomharibia jina.

“Mimi ni msichana mzuri sana unajua, usijaribu kunichomea,” Edday aliandika akiweka emoji za kucheka.

Hii ni mara ya kwanza wawili hao kuonekana wakifanyiana utani wa kimahaba mitandaoni, mwezi mmoja baada ya Nderitu kuweka bayana katika maelezo marefu kwamba hawezi kubali kuingia katika ndoa ya wake wawili, akilenga mkuki kwa Seneta Nyamu ambaye amemteka Samidoh kwa mapenzi yasiyojua kufa.

Ndritu alisema kwamba anaona mwisho wa ndoa yake na mwanamuziki huyo wa Mugithi ambayo imedumu kwa miaka 15.

Hivi juzi baada ya Nyamu kuonekana na Samidoh katika hafla ya waziri Moses Kuria, Nderitu alipakia video akidokeza kwamba yuko singo, licha ya kutoweka wazi iwapo kweli ameamua kuachana kabisa na Samidoh au wanaendelea kutafuta mwafaka mbali na kamera za mapaparazzi.

Baadhi walisema kwamba wanasubiri kusikia kutoka kwa Karen Nyamu pindi atakapoona tukio hili jipya.