Nyamu kuhusu kumzalia Samidoh, "Baba mzuri anastahili watoto wengi"

Karen alikiri kwamba Samidoh ni baba mzuri na fadhila yake ni kuzaliwa watoto wengi kama shukrani ya uzuri wake.

Muhtasari

• Ni kiashiria tosha kuwa Samidoh amefanikiwa kupata suluhu la furaha katika wake zake wote wawili, kila mmoja akifurahia kuwa naye kwa wakati wake.

Karen Nyamu akiwa na Samidoh katika tukio la bintiye.
Karen Nyamu akiwa na Samidoh katika tukio la bintiye.
Image: Facebook

Seneta Karen Nyamu, mke wa pili wa msanii wa Mugithi na afisa wa polisi Samidoh ni mtu anayejulikana kwa ushindani mwingi.

Wikendi iliyopita baada ya mke wa kwanza Edday Nderitu kupakia picha kadhaa kutoka kwa tukio kubwa la kusherehekea siku ya kuzaliwa na mwanawe na mwanamuziki huyo, Jumapili usiku Nyamu naye alijibu mipigo kwa kupakia picha kutoka kwa tukio la siku ya kuzaliwa ya bintiye na Samidoh.

Kitendo cha Nyamu kilitafsirirwa na wengi kama kujaribu kufunika kabisa tukio la Edday lisizungumziwe, ili yeye abaki kuwa gumzo pekee katika mzunguko wa maisha ya Samidoh.

Hata hivyo, Nyamu alisindikiza picha hiyo na kapsheni ya kujitetea, akisma kwamba ni kutokana na shinikizo la umma.

Pia alidokeza kwamba hana ubaya na tukio la mtoto wa Edday kusherehekea siku yake ya kuzaliwa wakiwa na Samidoh, akidokeza kwamba Samidoh ni baba mzuri na kwa hivyo anastahili kuwa na watoto wengi.

“Sawa kutokana na mahitaji ya umma hehehe. Baba mzuri anastahili watoto wengi. Heri ya kuzaliwa Neriah Muchoki,” Karen Nyamu alipakia.

Katika tukio kubwa la mtoto wa Edday, wengi walishangaa kumuona Samidoh akiwa pale kushuhudia mtoto wake akiongeza mwaka mwingine maishani, kwani hili halikutarajiwa kutokana na misukosuko ambayo wawili hao wamekuwa wakipitia, Edday akichukizwa na hatua ya Samidoh kuonekana mara kwa mara na Nyamu licha ya kuomba radhi kuwa hilo halingetokea.

Samidoh ni baba mzuri kwa wanawe, na amelionesha hilo kwa kuhakikisha anatokea katika matukio makubwa ya wanawe kutoka pande zote – kwa Edday na kwa Nyamu.

Watumizi wengine wa mitandao ya kijamii walihisi kwamba hatimaye Samidoh amefanikiwa kumaliza uhasama uliokuwa umeonekana baina ya wake zake, huku ikionekana kama wote sasa wana furaha na kila mmoja kwa namna yake amekubali kuwa Samidoh huenda hayuko tayari kumuacha mmoja kwa ajili ya mwingine. Ni kubanana tu kwenye huba la mitala.