Binamu wa Samidoh amtupia bomu Karen Nyamu kwa kumpenda 'mume wa mtu'

Kuchumbiana na mume wa mtu ni sawa sawa na kujiingiza katika ulimwengu wa ushindani kila wakati - Saroni aliandika.

Muhtasari

• Saroni alisema kuwa yeye katu hawezi toka kimapenzi na mume wa mtu kwani kufanya hivyo kunakufanya kuwa na chuki zisizo na sababu.

Nyamu ashambuliwa na binamu wa Samidoh
Nyamu ashambuliwa na binamu wa Samidoh
Image: Facebook

Bernice Saroni, binamu wa nyota wa Mugithi Samuel Muchoki aliyefahamika kwa jina la usanii Samidoh, amemkashifu Karen Nyamu kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume aliyeoa.

Katika ujumbe unaoonekana kuelekezwa kwa seneta mteule ambaye yuko kwenye uhusiano haramu na mwanamuziki huyo, Saroni anasema kuwa na mwanamume aliyeoa ni sawa na kuwa katika ulimwengu wa ushindani.

Binamu ya Samidoh anadai zaidi kwamba mwanamke huyo atapigania nafasi yake kila wakati. Anaitaja kuwa na uzoefu mbaya zaidi maishani.

"Jambo baya zaidi ni kuchumbiana na mwanamume aliyeoa, utakuwa katika ulimwengu wa ushindani kila wakati," aliandika kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook.

Bernice alisema hatawahi kuwa mwanamke katika uhusiano au uchumba na mwanamume aliyeoa, kwake, hiyo ni njia ambayo hawezi kuchukua.

"Halafu wivu weeeeh...siwezi," ujumbe ulisomeka zaidi.

Hii si mara ya kwanza kwa Saroni ambaye anaishi Marekani anaonesha kutofurahishwa kwake na kitendo cha Nyamu kutoka kimapenzi na Samidoh, jambo ambalo limeonekana kukwamisha uhusiano wa Samidoh na mke wake wa kwanza Edday.

Zogo lake na Nyamu lilianza mwaka jana pale ambapo Samidoh alielekea Marekani kwa ziara yake ya kimuziki na Saroni alikuwa mwenyeji wake lakini Nyamu akawa na mawazo mtanange kuwa ni mwanamke ambaye alikuwa anajaribu kutoka kimapenzi na Samidoh.

Hivi majuzi, Edday alizungumzia uwezekano wa kuwa katika ndoa ya wake wawili, akibainisha kwamba kuna tofauti ya mwanamume mwenye wake wawili na kuhanya nje ya ndoa, alikuwa anamjibu shabiki mmoja aliyemsifia Samidoh katika moja ya machapisho yake.

Kulingana na hali ya wasifu wa Saroni, yeye ni Mtaalamu wa Afya ya Akili anayefanya kazi katika Kituo cha Jeraha la Kiwewe huko Lowell, Massachusetts.