Akaunti ya Twitter ya DJ Moh yadukuliwa

Alhamisi, huduma muhimu zinazotolewa na mashirika ya serikali yaliathirika baada ya kudukuliwa.

Muhtasari

• Dj huyo akizungumza na Nairobi News alifichua kuwa akaunti hiyo imedukuliwa kwa zaidi ya wiki tatu sasa.

• DJ Moh, alisema akaunti hiyo ilikuwa ya muhimu sana katika kazi yake hata kama hakuwa akiitumia sana bado aliihitaji kuweza kuwafikia mashabiki wake katika mtandao huo.

Akaunti ya Twitter ya DJ Moh yadukuliwa.
Akaunti ya Twitter ya DJ Moh yadukuliwa.
Image: INSTAGRAM/DJ MOH

Akaunti ya Twitter ya mcheza santuri na mume wa mwanamziki Size 8, DJ Moh yenye zaidi ya mashabiki zaidi ya 100,000 imedakuliwa.

Dj huyo akizungumza na Nairobi News akitafuta usaidizi kutoka kwa yeyote anayeweza kumsaidia kurejesha akaunti yake, alifichua kuwa akaunti hiyo imedukuliwa kwa zaidi ya wiki tatu sasa.

Kulingana na baba huyo wa watoto watatu, akaunti yake ilidakuliwa baada ya kusahau kulipia Doamin anayotumia katika akaunti yake ya Twitter na hivyo kumlazimu mwmiliki wa Domain ile kuipiga mnada.

“Nilicheleweshwa kurenew domain yangu, nalipa karibu Sh4000. Nadhani nilisahau, kisha mwenye domain akaitoa kwa watu wa kawaida ambao waliinunua na nadhani hivyo ndivyo wanaimiliki akaunti hiyo walivyoipata,"alisema.

DJ Moh, alisema akaunti hiyo ilikuwa ya muhimu sana katika kazi yake hata kama hakuwa akiitumia sana bado aliihitaji kuweza kuwafikia mashabiki wake katika mtandao huo.

“Sijapata mtu wa kunisaidia kuishughulikia. Sikuwa mtu wa Twitter, lakini ninaihitaji sana. Yeyote anayeweza kunisaidia kuipata, nitashukuru,” DJ Mo alisema.

Tukio hili la kusikitisha si mara ya kwanza kwa DJ Mo kukumbana na udakuzi mitandaoni. Miaka ya hapu nyuma, akaunti yake ya Facebook ilidakuliwa. Hata hivyo, aliweza kuwasiliana na ofisi za Facebook nchini Uingereza na kuweza kurudishiwa akaunti hiyo.

Alhamisi, huduma muhimu zinazotolewa na mashirika ya serikali ikiwa ni pamoja na tuvuti ya e-Citizen, Huduma za ununuzi wa token za KPLC, shirika la reli nchini, NTSA, Mpesa,Benki ya Standard Chartered na benki ya ABSA yaliathirika baada ya kudukuliwa na watu wanaodaiwa kuwa kutoka Sudan.

Waziri  Eliud Owalo alithibitisha shambulio katika huduma za e-Citizen lakini akasema hakuna data iliyoathiriwa. Huduma katika tuvuti hiyo hata hivyo ziliweza kurejeshwa baada ya wataalamakatika wazara ya ICT kuingililia kati.

Alhamisi jioni, Kampuni ya Kenya Power and Lighting ilisema mfumo wake ulikumbwa na hitilafu ya mtandao na kusababisha kutopatikana kwa baadhi ya huduma ikiwa ni pamoja na ununuzi wa token kutumia USSD na Mpesa.