Jamaa adai Burna Boy alitoa uume wake kafara kwa shetani ndio maana hana mtoto

Jamaa huyo alidai kwamba msanii hiwezekani msanii huyo mwenye mafanikio makubwa akiwa na miaka 30 bila hata mtoto mmoja wa kusingiziwa.

Muhtasari

• Jamaa huyo alizua dhana kwamba huenda Burna Boy alitoa uume wake kafara kwa shetani ili kupata mafanikio kimuziki.

Burna Boy
Burna Boy
Image: Instagram

Bayo Otedola, mtumiaji wa X amezua hasira kwenye jukwaa baada ya kuanzisha mjadala kumhusu msanii Burna Boy.

Otedola alikuwa anajibu tweet moja iliyowataka watumizi wa jukwaa hilo kuanzisha mjadala wa kuzua utata.

Hapo Otedola aliona fursa hiyo kutema nyongo ya kile ambacho amekuwa akikifikiria kwa muda mrefu kuhusu Burna Boy.

Alidai kwamba Burna Boy mwenye umri wa miaka 30 ni kinaya kikubwa sana kwani haiwezekani mtu mwenye umri kama huo na umaarufu wote asiwe hana mtoto hana yule wa kusingiziwa tu.

Jamaa huyo alizua dhana kwamba huenda Burna Boy alitoa uume wake kafara kwa shetani ili kupata mafanikio kimuziki pamoja na umaarufu ndio maana hana hata mrembo wa kusema kwamba ndiye mpenzi wake, Zaidi ya kuonekana karibu na mamake mzazi muda mwingi.

Aliandika kwenye Twitter, "Burna Boy alitoa kafara uanaume wake, kwa nini mtu wa miaka 30 akose mtoto?"

Tweet hii imevutia maoni tofauti kutoka kwa watumiaji wengine wa Twitter na tunatumai kuwa Burma Boy haitaiona.