Diamond hawezi kufanya shoo yoyote chini ya Ksh 14.3M - Meneja Sallam SK afichua

“Kama unatengeneza jukwaa na hali ya juu la shilingi milioni 200, kwa nini msanii anayeenda kupanda kwenye steji ya asilipwe milioni 200 vile vile?" SK alihoji.

Muhtasari

• “Hela za Diamond kupiga shoo mbona inajulikana tu. Inategema lakini si chini ya dola laki moja [shilingi za Kenya milioni 14.3],” alisema

Sallam SK
Sallam SK
Image: Screengrab

Meneja msimamizi wa kazi za Sanaa za msanii Diamond Platnumz, Sallam SK amefichua kiasi cha hela ambacho Diamond analipwa kwa kila shoo anayoifanya.

SK ambaye alitokea kwenye kipindi cha Jana na Leo kwenye Wasafi FM Jumatano alisema kwamba msanii huyo kuanzia mwezi wa tano mwaka huu atakuwa na mfululizo wa shoo, huku akifichua kiasi cha hela anayolipwa kwa kila shoo.

“Hela za Diamond kupiga shoo mbona inajulikana tu. Inategema lakini si chini ya dola laki moja [shilingi za Kenya milioni 14.3],” alisema

Meneja huyo ambaye pia ni mmiliki wa chombo cha redio alisema kwamba inastahili hivyo kwa kuangalia ukubwa wa Diamond na timu nzima anayopanda jukwaani nayo.

“Kuchua kiasi kidogo haiwezekani kwa sababu unajua inapofika kwenye gharama, umepanda kwenye steji na watu 20-30 halafu tuseme unafanya shoo kwa milioni 10 [za Tanzania] hawa wengine unawalipa nini?” aliuliza.

“Kama unatengeneza jukwaa na hali ya juu la shilingi milioni 200, kwa nini msanii anayeenda kupanda kwenye steji ya asilipwe milioni 200 vile vile? Kwa hiyo hitaji sio tu kuhusu kiingilio pale mlangoni, hitaji Zaidi lipo pale kwamba mtu anapopanda pale kwenye jukwaa yeye ni chapa, kama anapanda juu, nini kinatakiwa kifanyike? Ndio maana unaona kuna biashara pale kwenye runinga. Kwa hiyo tunatakiwa kabisa tujue soko tunalifanyaje ili msanii aweze kua,” SK alibainisha.