“Alikuwa kama soulmate wangu!” Manzi wa Meru kuhusu kuchora tattoo ya Brian Chira mgongoni

“Brian Chira alikuwa kama soulmate wangu, naweza sema hivyo. Chira alikuwa kama roho yangu, nilikuwa nampenda sana, kwa hiyo niliamua kufanya hivyo kutokana na mapenzi ambayo nilikuwa nayo kwa Chira,” Magambo alisema.

Muhtasari

• Akizungumza na KOM, Magambo alisema kwamba alichora tattoo hiyo ili kuendelea kumuenzi Chira akimtaja kama ‘mwenzi wa rohoni’.

• Magambo alisema kuwa kuweka tattoo ya Chira kulikuwa kama mbadala ya tiba kwa uchungu wa kuondokewa na rafiki wake wa karibu

Manzi wa Meru na tatoo ya Brian Chira.
Manzi wa Meru na tatoo ya Brian Chira.
Image: Screengra// KOM (YouTube)

Jude Magambo, maarufu kama Manzi wa Meru amefichua sababu ya kuchora tattoo ya tiktoker marehemu Brian Chira katika mgongo wake.

Magambo ambaye anajionea fahari kuwa mwanachama wa LGBTQ wiki jana alichora tattoo ya Brian Chira kwenye mgongo wake ikijumuisha picha yake na tarehe alipofariki.

Akizungumza na KOM, Magambo alisema kwamba alichora tattoo hiyo ili kuendelea kumuenzi Chira akimtaja kama ‘mwenzi wa rohoni’.

“Brian Chira alikuwa kama soulmate wangu, naweza sema hivyo. Chira alikuwa kama roho yangu, nilikuwa nampenda sana, kwa hivyo nikaona ni kama atatoweka kabisa katika muda wa kipindi kifupi na uchungu ambao nimekuwa nikihisi mpaka leo ni Zaidi, hivyo nikahisi kwamba hiyo tattoo itamaliza huo uchungu, na nina furaha uchungu unaendelea kuisha kadri muda unavyosonga, kwa hiyo niliamua kufanya hivyo kutokana na mapenzi ambayo nilikuwa nayo kwa Chira,” Magambo alisema.

Magambo alisema kuwa kuweka tattoo ya Chira kulikuwa kama mbadala ya tiba kwa uchungu wa kuondokewa na rafiki wake wa karibu na akasema kwamba ni kweli tangu alipoichora wiki jana, ameona matokeo kwani uchungu huo umeanza kupungua.

“Kusema kweli inafanya kazi vizuri, ni kama njia sahihi ya kumuomboleza Chira kwa sababu wakati wowote ninapooga namuangalia kwenye mwili wangu, nafarijika na kuhisi vizuri,” alisema akithibitisha kwamba ni tattoo ya kweli wala si ya kuchora na wino.

Manzi wa Meru alisema kwamba wakati wa kuchora tattoo hiyo, alihisi uchungu sana lakini aliweka nadhiri kwamba angevumilia kutokana na kina cha mapenzi aliyokuwa nayo kwa marehemu Brian Chira.

Kuhusu ni kwa nini alichagua kuichora tattoo hiyo upande wa mgongo na si sehemu nyigine ya mwili, Manzi wa Meru alisema;

“Nilihisi kwamba hiyo sehemu [mgongoni upande wa juu] ni sehemu tosha, na hapa mbele [kweney kifua] nilikuwa natamani kuchora tattoo ya pengine mamangu siku zijazo, kwa hivyo nikaona acha niiweke kwa mgongo kwa sababu haingetoshea kwa upande wa mkono.”

“Nimechora jina la Brian Chira, picha yake na tarehe alikufa. Kwangu hiyo tattoo ni kubwa sana kwangu na ndio ya kwanza kubwa kwenye mwili wangu, zingine ni ndogo ndogo tu za maandiko. Na sidhani kuna nyingine itaweza zidi hiyo kwa ukubwa,” Magambo alieleza.

Pia aliweza kuzungumzia kuhusu gharama ya tattoo hiyo na muda ilimchukua kuchorwa.

“Tatoo ya Chira kwenye mwili wangu ilinigharimu sana, kwa sababu kwanza singeenda kuchorwa na mtu ambaye hajui kitu, ni ghali sana lakini machoni pa Chira hakuna kitu ghali kwa sababu akiwa hai tulikuwa tunafanya vitu hata ghali zaidi,” alisema.