"Kurekodi uchi wa wengine ni ukiukaji wa sheria" KFCB

Ujumbe huu unafuatia kitendo cha kusambazwa kwa video mbili chafu ambazo zinazodaiwa kuwa za watu mashuhuri nchini.

Muhtasari

•"Kurekodi uchi wa wengine na idhini  yao au bila ni ukiukaji wa sheria ya filamu na michezo ya jukwaani

• Kipengele cha 222 kinasema hakuna filamu ya kuonyeshwa umma ambayo itatengenezwa bila leseni ya kucheza filamu" Mutua aliandika.

Dr Ezekiel Mutua
Dr Ezekiel Mutua
Image: Hisani; KFCB

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya uainishaji filamu nchini (KFCB) Daktari Ezekiel Mutua amelaani kitendo cha watu kurekodi uchi wa wenzao bila idhini.

Kupitia mtandao wa Twitter, Mutua amesema kuwa kitendo hicho ni haramu kulingana na katiba ya Kenya.

"Kurekodi uchi wa wengine na idhini  yao au bila ni ukiukaji wa sheria ya filamu na michezo ya jukwaani kipengele cha 222 kinachosema hakuna filamu ya kuonyeshwa umma ambayo itatengenezwa bila leseni ya kucheza filamu" Mutua aliandika.

Ujumbe huu unafuatia kitendo cha kusambazwa kwa video mbili chafu ambazo zinazodaiwa kuwa za watu mashuhuri nchini. 

Siku chache zilizopita, mwanasoshalaiti mmoja nchini alijipata pabaya baada ya video iliyomuonyesha akivaa nguo  kuenezwa mitandaoni.

Msichana mmoja anadaiwa kurekodi video isiostshili ya mwanasiasa nchini hatua ambayo imezua mjadala mkali nchini.

"Je, ni kweli? ni vyema? ni lazima?" Mutua aliuliza kuhusiana na kuenezwa kwa video chafu.

(Mhariri: Davis Ojiambo).