'Nakupenda,huwezi kuzuilika,'Brown Mauzo amwambia Vera Sidika anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti maarufu nchini Vera Sidika, anasherehekea siku yake ya kuzaliwa hii leo, huku akihitimu mika 32
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti maarufu nchini Vera Sidika, anasherehekea siku yake ya kuzaliwa hii leo, huku akihitimu mika 32.

Sidika amekuwa akivuma sana mwaka huu baada ya kutangaza kwamba ana ujauzito na msanii Brown Mauzo.

Huku Mauzo akisherekea siku ya kuzaliwa ya mkewe, alimwandikia ujumbe wa kiekee na kumsifia jinsi alivyo mrembo, na kumhakikishia kwamba anampenda.

"Napenda tabasamu yako, napenda mguso wako,napenda mtazamo wako,napenda mwili wako, nakupenda, huwezi kuzuilika, heri njema siku yako ya kuzaliwa mke wangu," Mauzo aliandika.

Baada ya Vera kuona ujumbe wake mumewe alimjibu na kumshukuru kwa kumpa ujauzito, na pia kushukuru kusherehekea siku yae ya uzaliwa akiwa naye.

"Asante sana mpenzi, inapendeza kusherehekea mwaka mwingine na wewe, na mwanadamu mwingine ambaye yuko ndani yangu, zawadi ya kipekee milele nakupenda," Vers Sidika alijibu.

Mauzo pia alimjibu na kumwambia kwamba hawezi subiri mtoto wao ili akamilishe familia yao ya kushangaza na enye furaha.

"Nashukuru kwamba ninasherehekea siku hii maalum na wewe,siwezi kusubiri malaika wetu mdogo kukamilisha familia yetu ya kushangaza yenye furaha."