Wajackoya atemwa na Justina Wamae baada kugura Chama cha Roots

Justina alieleza kwamba anajiuzulu kwenye chama hiyo kwa hiari yake.

Muhtasari

• Justina na Wajackoya waliwania katika uchaguzi mkuu wa 2022 na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kinyang'anyiro cha urais.ote wakisimamiwa na chama chao cha Roots.

Viongozi wa chama cha Roots.
JUSTINA WAMAE, GEORGE WAJACKOYAH Viongozi wa chama cha Roots.
Image: Maktaba

Aliyekuwa mgombea mwenza wa Profesa George Wajackoya, Justina Wamae amejiuzulu kwenye chama cha Roots.

Justina na Wajackoya waliwania katika uchaguzi mkuu wa 2022 na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kinyang'anyiro cha urais. Wote wakisimamiwa na chama chao cha Roots.

Kwenye mtandao wake wa Twitter Justina alieleza kwamba anajiuzulu kwenye chama hiyo kwa hiari yake.

Wamae alisema kumekuweka na uhasama baina yake na  Wajackoya kutokana na uwezo wa chama hicho kupokea ufadhili wa serkali. Alisema chama cha Roots hakifuzu kupokea fedha za vyama.

 

Uhasama uliyokuwa kati yake na mkubwa wake na hali ya chama hicho kutoweza kunufaika na hazina ya vyama kisiasa pia vilichangia kugura kwake kutoka Roots Party.

“Wanaweza kula hewa lililo na joto. Tazama,”alisema Justina.

Aliweza kuambatisha barua yake ya kujiuzulu aliyomtumia katibu kuu wa chama cha Roots.

Barua hiyo ilieleza kuwa jukumu lake Justina la kuwa mgombea mwenza wa Wajackoya  lilifika hitimisho Rais William Ruto alipotangazwa rais wa Kenya. Hii ni baada ya Justina kutoa maoni yake kuhusu mkutano wake Rais William Ruto na Waziri mkuu wa Jamaika.

Justina alimuomba Rais kuhalalisha katani bangi.

“halalisha bangi,”alisema.

Chama cha Roots kilipata sifa zake wakati wa kampeni za kuomba kura wakitaka kilimo cha bangi kuhalalishwa.

Katika mdahalo wa wagombea wenza , Wamae alifichua kwamba Roots ilikua inataka kulalisha dhambi.