Martha Koome: Ushahidi wa Julie Soweto kuhusu Jose Carmago ni uvumi tupu

Jaji Koome alipuuzilia mbali kwamba madai hayo hayakuwa na ushahidi.

Muhtasari

• Akisoma uamuzi wa jopo la majaji saba wa mahakama ya upeo, Koome alisema kwamba madai hayo ya Soweto yalikuwa ni uvum

Jaji wa mahakam ya juu Martha Koome
Jaji wa mahakam ya juu Martha Koome
Image: maktaba

Jaji Martha Koome, rais wa idara ya mahakama nchini Kenya amepuuzilia mbali madai yaliyoibuliwa na wakili wa upande wa malalamishi, Julie Soweto kwa kusema kwamba kulikuweko na mtu kwa jina Jose Camargo katika seva za IEBC ambaye aliamua uchaguzi wa Agosti 9.

Akisoma uamuzi wa jopo la majaji saba wa mahakama ya upeo, Koome alisema kwamba madai hayo ya Soweto yalikuwa ni uvumi tu ambao haukuwa na ushahidi wa kutosha kudhibitisha uwepo wa mtu huyo aliyetajwa kuwa raia wa Venezuela.

"Ushahidi uliotolewa na wakili Julie Soweto (kwenye Jose Carmago) ulithibitika kuwa si chochote zaidi ya hewa moto," alisoma Koome.

Jaji huyo pia alisema kwamba jopo lake lilibainisha kwamba hakukuwa na uhusiano wowote kati ya kuahirishwa kwa kura katika baadhi ya maeneo na kufifisha kura za Raila Odinga.

Mahakama ya Juu ilisema hakuna ushahidi kwamba kuahirishwa kwa uchaguzi wa Mombasa, Kakamega na maeneo mengine sita kote nchini kulisababisha ukandamizaji wa wapiga kura na kumsababishia Raila Odinga.