Watu 230 wauawa Sudan Kusini kwenye mzozo wa mifugo

Muhtasari

• Mamlaka nchini Sudan Kusini zimesema zaidi ya watu 230 wameuawa katika muda wa wiki mbili zilizopita katika mapigano ya kikabila kusini mwa nchi hiyo.

Image: BBC

Mamlaka nchini Sudan Kusini zimesema zaidi ya watu 230 wameuawa katika muda wa wiki mbili zilizopita katika mapigano ya kikabila kusini mwa nchi hiyo.

Mzozo kuhusu ng'ombe na mashamba ya malisho ulitokea katika jimbo la Ikweta Mashariki kuanzia mapema mwezi huu. Mauaji hayo yametokea katika kaunti ya Kapoeta Kaskazini ambapo jamii hasimu zilipambana kufuatia uvamizi wa mifugo katika mojawapo ya vijiji hivyo.

Waliouawa ni pamoja na chifu wa eneo hilo ambaye alipigwa risasi. Gavana wa jimbo hilo amelaani mauaji hayo na kuiomba serikali kutuma haraka vikosi vya usalama katika eneo hilo ili kusaidia kurejesha hali ya utulivu.

Ilikuja wakati Sudan Kusini inaadhimisha miaka 11 ya uhuru. Umoja wa Mataifa umeonya kuwa nchi hiyo iko katika hatari ya kurejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mapigano baina ya jamii ambayo yamesababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.