Mshukiwa aliyetoweka na Sh11 milioni atafutwa na DCI

Maafisa wapelelezi wa jinai wanamsaka mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuvunja na kuiba kiasi hicho cha pesa

Muhtasari
  •  Inadaiwa Mshukiwa kuiba pesa hizo kwa Kuvunja Kabati ambapo hizo pesa zilikuwa zimewekwa na kutoweka nazo
Abdirizack Moktar Garat, jamaa anayetuhumiwa kuiba pesa Estleigh
Abdirizack Moktar Garat Abdirizack Moktar Garat, jamaa anayetuhumiwa kuiba pesa Estleigh
Image: DCI (FACEBOOK)

Maafisa wa upelelezi wanamsaka Abdirizack Moktar Garat kuhusiana na kutoweka kwa takriban Sh11 milioni kutoka kwa Jengo la Salama Center, huko Eastleigh.

Inadaiwa Mshukiwa kuiba pesa hizo kwa Kuvunja Kabati ambapo hizo pesa zilikuwa zimewekwa na kutoweka nazo. Katika taarifa, DCI inawaomba wananchi walio na taarifa zozote kuhusiana na aliko kujitokeza na kuripoti.

Picha za Mshukiwa zimesambazwa kwenye Mitandao ya kijamii kufahamisha umma kumhusu kama mtu ambaye hafaikutangamana na watu.

“DCI inawaomba wananchi kwa taarifa zozote zinazoweza kusababisha kukamatwa kwa mshukiwa ambaye amejificha. Ikiwa una habari yoyote kuhusu aliko, tafadhali wasiliana nasi kupitia nambari yetu ya simu 0800722203,” DCI ilisema.

Maafisa wa upelelezi walisema alijificha baada ya madai ya wizi na msako wa kumtafuta kuanzishwa.Maafisa wa upepelezi sasa watashirikiana na umma haswa wakaazi wa Eastleigh kuhakikisha kuwa mshukiwa ambaye yuko mbioni kushikwa na kufunguliwa mashtaka.

Visa kama hivi zimekuwa zikiongezeka kitu ambacho sasa Serikali imeamua kupambana nayo, kwa msingi ya kuikomesha.