DP Rigathi Gachagua amtuza mwanadada aliyevumbua jina 'Riggy G'

Chelimo alitoa shukrani kwa Naibu Rais kwa kumpatia kazi katika ofisi yake

Muhtasari

• Naibu Rais alimpongeza Ivy Chelimo kwa kuwa mbunifu kwa kumpa kazi katika ofisi yake ya Harambee.

Rigathi Gachagua na Ivy Chelimo

Naibu wa Rais William Ruto, Rigathi Gachagua alimtambua mwanadada aliyebuni jina lake la utani la Riggy G.

Gachagua alimwalika  Ivy Chelimo kuandamana naye katika halfa ya kuadhimisha Vyakula duniani iliyofanyika huko Kajiado.

Naibu Rais alitangaza kwenye hafla hiyo kuwa amemtunuku kazi mwanadada huyo  katika serikali kwa kumpa jina la utani.

Alimpatia kazi katika ofisi yake ya Harambee kama alivyoahidi hapo awali.

Gachagua alimkaribisha Chelimo kutoa hotuba kuhusu hafla hiyo kueleza hisia zake baada ya kupata kazi ya serikali.

 Gachagua alipomkaribisha Chelimo kutuo hotuba kwa umma, mwanahabari alionekana kutaka kubadilisha kipaza sauti.

Alijaribu kubadilisha kipaza sauti alichokuwa akitumia Naibu Rais ili ampatie Chelimo kingine cha kutumia.

Naibu Rais alionekana kupinga jambo hilo na kumwambia mwanahabari huyo amuache Chelimo atumie kipaza sauti chake.

"Ah wacha atumie hii," Gachagua alimwambia mwanahabari huyo.

Chelimo alitoa shukrani kwa Naibu Rais kwa kumpatia kazi katika ofisi yake kama njia ya kuwainua vijana.

Alisema kuwa Gachagua ana nia ya kuwahamasisha vijana kuwa viongiozi wa kesho na hilo litaanza na yeye.

Chelimo alisema kuwa Gachagua anahakikisha kuwa vijana watapata kazi katika serikali ili waweze kuelewa jinsi serikali inavyofanya kazi yake.