RIP:Mwanahabari wa NTV Elizabeth Mareb afariki akiwa na umri wa miaka 31

Merab kwa miaka mingi amekuwa akipambana na ugonjwa wa seli Mundu hali ambayo alipatikana nayo akiwa na umri wa miaka 10.

Muhtasari

• Mzaliwa wa kwanza katika familia ya watu watano ni mtu wa pili kwenye familia yake kufa kutokana na Sickle Cell.

• Kulingana na Nation Mnamo 2019, Merab aligunduliwa kuwa na ugonjwa unaojulikana kama Vascular Necrosis.

Mwanahabari wa NTV afariki baada ya kuugua seli mundu.
KIFO Mwanahabari wa NTV afariki baada ya kuugua seli mundu.
Image: Hisani

Mwanahabari wa afya wa NTV Elizabeth Merab amefariki dunia.

Merab kwa miaka mingi amekuwa akipambana na ugonjwa wa seli Mundu hali ambayo alipatikana nayo akiwa na umri wa miaka 10.

Aliaga dunia katika Hospitali ya The Aghakan, Nairobi akiwa na umri wa miaka 31 Jumamosi 15, Julai 2023.

Merba alilazwa kwa mara ya kwanza Jumanne, wakati huo alikuwa na maumivu makali.

Kulingana na jamaa yake, kwa wakati mmoja aliwekwa katika HDU.

Mzaliwa wa kwanza katika familia ya watu watano ni mtu wa pili kwenye familia yake kufa kutokana na Sickle Cell.

Dada yake alikuwa ameaga dunia kutokana na ugonjwa huo.

Kulingana na Nation Mnamo 2019, Merab aligunduliwa kuwa na ugonjwa unaojulikana kama Vascular Necrosis.

Hii ilitokea baada ya kugundulika kuwa hana Wengu. Hii ilipelekea mguu wake kukatwa.

Kulingana na NHS Wengu ni kiungo cha ukubwa wa ngumi kinachopatikana upande wa juu kushoto wa fumbatio lako, karibu na tumbo lako na nyuma ya mbavu zako za kushoto.

Majukumu ya wengu ni pamoja na

 - Kuchuja damu kwa kuondoa taka za seli na kuondoa seli za damu zilizozeeka au zilizoharibiwa.

 - Kutengeneza seli nyeupe za damu na kingamwili zinazokusaidia kupambana na maambukizi.

 - Kudumisha viwango vya maji katika mwili wako.Kuzalisha kingamwili zinazokukinga dhidi ya maambukizi.

Apumzike kwa amani.