Kericho: Kijana wa miaka 24 ajitoa uhai baada ya kupoteza 120K kwa Kamari ya Aviator

Kabla ya kifo chake, kijana huyo kwa jina Kipkorir aliajiriwa kuendesha duka la Mpesa ndani ya mji wa Kericho. Inaripotiwa kuwa alitumia pesa za biashara kujaribu bahati yake na kupoteza dau lake katika michezo yote.

Muhtasari

• Kabla ya kifo chake, kijana huyo kwa jina Kipkorir aliajiriwa kuendesha duka la Mpesa ndani ya mji wa Kericho.

• Inaripotiwa kuwa alitumia pesa za biashara kujaribu bahati yake na kupoteza dau lake katika michezo yote.

Kitanzi
Kitanzi
Image: HISANI

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 24 alipatikana amejinyonga na mwili wake kuning’inia kutoka kwenye paa la nyumba ya kukodisha baada ya kile kilichotajwa kuwa ni kupoteza hela nyingi kwenye mchezo wa bahati nasibu.

Kwa mujibu  wa NTV Kenya, kijana huyo alisemekama kuchukua uamuzi huo mgumu baada ya kupoteza hadi kiasi cha shilingi laki moja na elfu 20 kwenye mchezo wa Kamari ya kungurumisha ndege maarufu kama ‘Aviator’.

Kabla ya kifo chake, kijana huyo kwa jina Kipkorir aliajiriwa kuendesha duka la Mpesa ndani ya mji wa Kericho.

Inaripotiwa kuwa alitumia pesa za biashara kujaribu bahati yake na kupoteza dau lake katika michezo yote.

Akiongea na NTV kwa njia ya simu mpwa wa marehemu alisema marehemu alimuomba rafiki yake amtunzie duka kwani alienda kufanya shughuli kadhaa mjini na atarejea hivi karibuni.

"Tulijaribu mara kadhaa kuwasiliana naye lakini hakuwa akijibu simu," alisema mpwa wake.

Kulingana na ripoti ya polisi, hakuna ujumbe wowote aliouacha kabla ya kujitoa uhai.

Mwili huo ulitolewa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Siloam ukingoja uchunguzi wa upasuaji wa maiti