Ufalme wa Uingereza wazungumzia madai ya Harry na mkewe Meghan

Muhtasari

• Ufalme ulisema "kumbukumbu zinaweza kutofautiana" lakini madai yaliyotolewa katika mahojiano yao na Oprah Winfrey "yatazingatiwa mno".

• Jumba la ufalme limesema akina Sussex "wanapendwa sana na familia".

Mtoto wa kifalme wa Uingereza Harry na mkewe Meghan.
Mtoto wa kifalme wa Uingereza Harry na mkewe Meghan.
Image: FILE

Maswala ya ubaguzi wa rangi  yaliyotolewa na Duke na Duchess wa Sussex "yanatamausha" na yatashughulikiwa na familia kwa faragha, hekalu ya Buckingham ilimesema.

Katika taarifa, ufalme ulisema "kumbukumbu zinaweza kutofautiana" lakini madai yaliyotolewa katika mahojiano yao na Oprah Winfrey "yatazingatiwa mno".

Meghan aliambia Winfrey, Harry alikuwa ameulizwa na mmoja wa jamaa wake ambaye alibana jina lake "vile “ngozi nyeusi” ya mwawe Archie itakuwa.

Jumba la ufalme limesema akina Sussex "wanapendwa sana na familia".

Shinikizo zilikuwa zikiongezeka kwenye Jumba la Buckingham kujibu baada ya Meghan – mwanachama wa kwanza wa familia ya kisasa ya kifalme mwenye asili ya kiafrika – kufichua usemi kuhusu rangi ya ngozi ya mtoto wao.

Prince Harry baadaye alimweleza Winfrey kwamba maoni hayo hayakutolewa na Malkia au Mtawala wa Edinburgh.

Taarifa hiyo, ambayo ilikuja siku moja na nusu baada ya mahojiano hayo kupeperushwa kwa mara ya kwanza huko Amerika, ilisema: "Familia nzima imesikitishwa kujua kiwango kamili cha jinsi miaka michache iliyopita imekuwa migumu kwa Harry na Meghan.

"Maswala yaliyoibuliwa, haswa yale ya rangi, yanatamausha. Hata ingawa huenda kumbukumbu zingine zikatofautiana, zitachukuliwa kwa uzito sana na zitashughulikiwa na familia kwa faragha."

Jibu la Buckingham lilikuja baada ya mikutano ya dharura iliyohusisha washiriki wa familia ya kifalme baada ya mahojiano ya kibinafsi na Sussex, ambao walizungumza kuhusu ubaguzi wa rangi, afya ya akili, vyombo vya habari na washiriki wengine wa familia ya kifalme.