MATIANG'I TAABANI

Wandani wa Ruto walaumu Matiang'i kwa vurumai uchaguzini

Wabunge toka bonde la ufa wamesema kuwa wanajadiliana hatua watakayomchukila Matiang'i bungeni iwapo hatajitokeza kueleza kuhusu vurugu hizo

Muhtasari

•Wabunge toka bonde la ufa wamesema kuwa wanajadiliana hatua watakayomchukila Matiang'i bungeni iwapo hatajitokeza kueleza

Oscar Sudi
Oscar Sudi
Image: maktaba

Wandani wa naibu rais kutoka eneo la bonde la ufa sasa wanamtaka waziri Fred Matiang’I kujitokeza na kueleza chanzo cha vurugu zilizojitokeza kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni.

Wabunge hao wamesema kuwa wanajadiliana hatua watakayochukua dhidi ya Matiang’i bungeni ijapo atakosa kujitokeza kueleza kiini cha vurugu.

Mbunge wa Keiyo ya Kusini, Daniel Rono na Bowen Kangogo wa Marakwet ya Mashariki walidai kuwa Matiangi alikuwa amepanga kutumia maafisa wa kulinda Amani kusababisha vurugu na kuiba chaguzi zilizofanyika.

Matiang’i amenyamaza  nay eye ndiye amesimamia wizara ya ulinzi, yafaa ajitokeze na aeleze Wakenya kilichotokea” Kangogo alisema.

Wabunge wale wawili waliokuwa wakiongea wakiwa Keiyo Kusini walisisitiza kuwa jambo hilo lisiposhughulikiwa huenda mambo yakaharibika mwaka ujao.

Mbunge wa Kapsaret, Oscar Sudi amesema kuwa wamekasirika naye Matiang’i, Karanja Kibicho na Inspekta mkuu Hillary Mutyambai. Sudi pamoja na viongozi wengine toka bonde la ufa waliwalaumu watatu hao kwa vurumai zilizojitokeza.

Sudi alidai kuwa Matiang’I aliwapeleka polisi wengi katika eneo la Bonchari na Juja akijaribu kuwatumia kuiba uchaguzi.

Sudi pia alikashifu rais Kenyatta kwa kukubali ukatili kuenezwa nchini huku akidai kuwa rais alitaka kutumia mchakato wa BBI kutimiza matakwa yake binafsi badala ya kustaafu na kuenda nyumbani.

Seneta wa Nandi, Samson Cherargei pia alisuta utumizi mbaya wa nguvu za polisi wakati wa uchaguzi.

"Hata mkitumia nguvu, Wakenya hawako tayari kwa hayo na ndio maana wakaasi katika eneo la Juja, Bonchari na kwingineko” Cherargei alisema.