JUBILEE YAJIBU

Ni uvumi tu! Jubilee yakanusha madai ya kujiuzulu kwa Murathe

Tangazo hilo limetokana na video inayozunguka mitandaoni ikimuonyesha Raphael Tuju akitangaza kupokea barua ya kujiuzulu kutoka kwake Murathe.

Muhtasari

•Tangazo hilo limetokana na video inayozunguka mitandaoni ikimuonyesha Raphael Tuju akitangaza kupokea barua ya kujiuzulu kutoka kwake Murathe.

•"Bwana Murathe anabaki kuwa naibu mwenyekiti wetu na anaendelea kutekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo kwa bidii ili kutimiza majukumu yake kama ilivyoandikwa kwenye katiba ya chama" Jubilee ilitangaza.

David Murathe
David Murathe

Chama tawala cha Jubilee kimekanusha madai kuwa naibu mwenyekiti, David Murathe amejiuzulu kutoka uongozi wa chama hicho.

Tangazo hilo limetokana na video inayozunguka mitandaoni ikimuonyesha katibu mkuu wa chama hicho, Raphael Tuju akitangaza kupokea barua ya kujiuzulu kutoka kwake Murathe.

Tangazo hilo lilitolewa kupitia ujumbe ulioandikwa na mkurugenzi wa mawasiliano pale, Albert Memusi na kuwekwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya chama hicho jioni ya Jumanne.

"Bwana Murathe anabaki kuwa naibu mwenyekiti wetu na anaendelea kutekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo kwa bidii ili kutimiza majukumu yake kama ilivyoandikwa kwenye katiba ya chama" Jubilee ilitangaza.

Chama hicho kimesihi uma kutupilia mbali ripoti zinazosema kuwa Murathe aliacha kazi yake. Kimesisisitiza kuwa matangazo rasmi yatatolewa kupitia njia rasmi ila si uvumi tu.

"Mawasiliano rasmi kuhusu mabadiliko katika chama yatazungumzwa kupitia njia rasmi kama ilivyo kawaida na kama ilivyoandikwa kwenye katiba ya chama" Memusi aliandika.

Chama hicho kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta kimekuwa kikikumbwa na misukosuko mingi ya kisiasa haswa baada ya kupoteza viti zote katika chaguzi ndogo zilizofanyika hivi majuzi.

Baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwanyooshea kidole cha lamama David Murathe na waziri Fred Matiang'i huku wakiwaagiza kujiuzulu ikiwemo Ngunjiri wambugu wa Nyeri.