MVUTANO TANGATANGA

Mgogoro Tangatanga:UDA yakanusha madai ya Moses Kuria

Chama cha UDA kimepinga madai ya Kuria kuwa kinaongozwa tu na wabunge wanaotawala ila si raia wa kawaida

Muhtasari

•Chama cha UDA kimepinga madai ya Kuria kuwa kinaongozwa tu na wabunge wanaotawala ila si raia wa kawaida

•Kimedai kuwa mgombeaji wake wa Kiambaa, Njuguna Wa Wanjiku, ni hasla mdogo na mtu aliyelelewa na mama peke

John Njuguna wa UDA
John Njuguna wa UDA
Image: Hisani

Chama cha United Democratic Alliance(UDA) kimepinga madai yaliyotolewa na Moses Kuria kuwa chama kile ni cha wabunge wanaotawala.

Kupitia ujumbe kwa wanahabari, chama hicho kimetangaza kuwa sio chake Johnston Muthama na hakiongozwi na wabunge kama alivyodai Moses Kuria alipokuwa anaondoa mgombeaji wake kwenye kinyang'anyiro cha Kiambaa.

"Kwa mara ya kwanza kuna uwakilishaji wa kimakusudi wa mahastla. Hii imeonyeshwa na chaguo letu huko Kiambaa na Muguga. Mgombeaji wetu Kiambaa, Njuguna Wa Wanjiku, ni hasla mdogo na mtu aliyelelewa na mama pekee" UDA ilisema kupitia katibu mkuu wa chama Veronica Maina.

ujumbe wa UDA
ujumbe wa UDA
Image: HISANI

Kwenye ujumbe huyo, chama cha UDA kilitangaza kuwa Omingo Magara alikuwa amegura chama cha People's Democratic Party(PDP) na kujiunga na UDA. Kilitangaza kuwa kimekuwa kikishirikiana na aliyekuwa waziri wa kilimo, Mwangi Kiunjuri kuhusu uteuzi wa wagombeaji.