Ruto: Tunamshukuru Mungu BBI ilishindwa

Muhtasari

• Naibu rais William Ruto alisema kubadilisha katiba kupitia BBI ilikuwa hatari kwa taifa. 

Naibu rais William Ruto
DP William Ruto Naibu rais William Ruto
Image: Maktaba

Jaribio la kubadilisha Katiba chini ya mchakato wa BBI ulikuwa mradi hatari zaidi katika historia ya Kenya, Naibu Rais William Ruto amesema.

 

Akizungumza siku ya Jumanne katika makazi yake mtaani Karen, naibu rais alisema mpango huo ungerejesha nyuma faida za kidemokrasia zilizopatikana Kenya tangu uhuru.

 

"Ilikuwa inakwenda kumsimamisha rais wa kifalme ambaye angeweza kudhibiti Mahakama, utenda kazi wa bunge. Ilikuwa hatari, ”naibu rais alisema.

“Tunamshukuru Mungu BBI ilishindwa. Tusijidanganye sisi wenyewe na watu, ”akaongeza.

 

Dkt Ruto alizungumza katika Makao yake ya Karen katika Kaunti ya Nairobi alipokutana na sehemu ya viongozi kutoka Kaunti ya Makueni.