•Hafla ya kuchoma mwili wa Njonjo ilifanyika takriban masaa matano baada yake kuaga dunia alfajiri ya Jumapili akiwa nyumbani kwake Muthaiga.
Habari na Gordon Osen
Mwili wa Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Kenya baada ya uhuru Charles Mugane Njonjo umechomwa katika chumba cha kuchomea maiti cha Kariokor.
Hafla ya kuchoma mwili wa Njonjo ilifanyika takriban masaa matano baada ya waziri huyo wa zamani wa Sheria na masuala ya Katiba kuaga dunia alfajiri ya Jumapili akiwa nyumbani kwake Muthaiga.
Hafla ya kumpungia Njonjo mkono ilihudhuriwa na wanafamilia wachache wa karibu.
Mwili wa Njonjo uliwasili katika chumba cha kuchomea maiti la Kariokor mwendo wa saa tatu unusu asubuhi ukisindikizwa na takriban wanafamilia 25.
Hafla ya kuchoma mwili wa marehemu ilianza kwa ibada fupi ya familia. Waandishi wa habari na watu waasio wa familia hawakuruhusiwa kuingia.
Njonjo aliaga dunia mwendo wa saa kumi na moja asubuhi ya Jumapili, Januari 1, 2022.
Marehemu ambaye alitambulika sana kama 'The Duke of Kabeteshire' alifariki akiwa na umri wa miaka 101.
Rais Uhuru Kenyatta amesherehekea marehemu kwa jukumu kubwa alilocheza katika ujenzi wa taifa na kwa kazi nzuri aliyofanya kwa kujitolea alipofanywa mwanasheria mkuu wa kwanza baada ya nchi kupata uhuru.