"Ndio serikali imekopa sana lakini haijafeli kulipa" - Kanze Dena

Muhtasari

• "Tunakopa tukiwa tunajua mahali tunawekeza fedha hizo ni mahali tutavuna mapato ili kupata hela za kulipa mikopo" - Kanze Dena atetea kukopa kwa Jubilee

Kanze Dena Mararo, msemaji wa Ikulu
Kanze Dena Mararo, msemaji wa Ikulu
Image: Screengrabs: YouTube

Msemaji wa ikulu Kanze Dena amepuuzilia mbali madai ya baadhi ya wanasiasa kwamba serikali ya rais Uhuru Kenyatta imekuwa ikilimbikiza madeni ya mikopo tu bila kuilipa.

Kanze Dena alisema haya siku ya Jumatatu katika mahojiano ya kipekee katika kituo kimoja cha redio nchini ambapo alisema kwamba serikali imekuwa ikijitahidi kulipa madeni ya mikopo kila mwaka.

Msemaji huyo wa ikulu alisema kwamba wale waanaoikosoa serikali kwamba inawatwika wakenya walipa ushuru mzigo mzito wa madeni si wakweli.

Alikubali kwamba kila mtu anajua serikali imekuwa ikikopa ili kuendesha shughuli muhimu za taifa katika kuanzisha miradi mbalimbali inayonuiwa kupanua uchumi na kusema kwamba tangu rais Kenyatta achukue hatamu za uongozi mwaka wa 2013, serikali yake haijawahi feli kulipa mikopo hiyo.

 

“Kumekuwa na kukopa lakini serikali haijawahi feli kurudisha mikopo hiyo. Tunakopa tukiwa tunajua mahali tunawekeza fedha hizo ni mahali tutavuna mapato ili kupata hela za kulipa mikopo,” alisema Dena.

Akiitetea serikali, Dena alisema kwamba bili ya mishahara na matumizi ya serikali yalipanda juu kutokana na serikali za ugatuzi ambazo zilitegemea pakubwa mapato kutoka serikali kuu.

Kanze Dena alilazimika kuanika wazi haya baada ya uvumi kusambazwa mitandaoni kwamba serikali ya Jubilee imeshindwa kulipa madeni ya mikopo iliyokopa kuanzisha miradi mbalimbali ya barabara kama ile ya Souther ByPass.

Tunakopa tukiwa tunajua mahali tunawekeza fedha hizo ni mahali tutavuna mapato ili kupata hela za kulipa mikopo,” alisema Dena.

Akiitetea serikali, Dena alisema kwamba bili ya mishahara na matumizi ya serikali yalipanda juu kutokana na serikali za ugatuzi ambazo zilitegemea pakubwa mapato kutoka serikali kuu.

Kanze Dena alilazimika kueleza wazi baada ya uvumi kusambazwa mitandaoni kwamba serikali ya Jubilee imeshindwa kulipa madeni ya mikopo iliyopata kuanzisha miradi mbalimbali ya barabara kama ile ya Souther ByPass.