Gavana Ngilu Amjibu Ruto Baada ya Kuongelea Ndoa Yake

Maoni hayo yalichochea matamshi ya Ruto kuhusu ndoa ya Ngilu.

Muhtasari

•Ruto alikuwa akimfanyia kampeni mgombeaji wa UDA wa ugavana Kitui Jonathan Mueke alipoonekana kumvamia Ngilu.

Gavana wa Kitui Charity Ngilu
Image: Musembi Nzengu

Gavana wa Kitui Charity Ngilu amemjibu Naibu Rais William Ruto baada ya kushambuliwa kwa uwezo wake wa kuoa.

DP ambaye alikuwa kwenye kampeni katika kaunti ya Kitui Jumanne aliwauliza wakaazi kuhusu alikokwenda Ngilu.

Alipokuwa akitangamana na wakaazi ambapo DP aliuliza ikiwa Ngilu anafaa kuolewa.

"Kwani mama mzee hivi anaweza kuolewa? Ataolewa na nani?'' Ruto aliuliza

Katika kumjibu, Ngilu ametaja matamshi ya DP kama dharau kwa wanawake wa Kenya.

Aliendelea kuongeza kuwa matamshi hayo yamedhihirisha jinsi gani hafai kwa uongozi.

''Ikiwa huwezi kuheshimu wanawake, huwezi kuheshimu mtu mwingine yeyote- Kwa sababu unafaa kujua kuwa ulitoka kwa mwanamke.William Ruto unaweza kutukana wanawake kila unavyotaka. Lakini katika uchaguzi huu, wanawake watatoa tamko kuu," aliandika kwa ukurasa wake wa Twitter

Ruto alikuwa akimfanyia kampeni mgombeaji wa UDA wa ugavana Kitui Jonathan Mueke alipoonekana kumvamia Ngilu.

"Na ule mama alienda aje?" DP aliuliza umati. Hapo ndipo sehemu ya umati ikijibu: “Alienda Bondo''.

DP kisha aliendelea kuuliza "Aliendaje Bondo, mlikataza yeye kura Alikwendaje Bondo, mlimnyima kura?" Swali la Ruto linarejelea hatua ya Ngilu kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha ugavana.

Mtu mmoja katika umati akamjibu kuwa ''Aliolewa Bondo".

Maoni hayo yalichochea matamshi ya Ruto kuhusu ndoa ya Ngilu.