Wambora na Lee Kinyanjui wakosa kuhudhuria kuapishwa kwa warithi wao

Tofauti na kaunti zingine ambapo watangulizi walikuwepo kukabidhi mamlaka

Muhtasari

• Katika kaunti hizo mbili kulikuwa na ushindani mkubwa sana

•Magavana wengi walikula kiapo Agosti 25.

Gavana Lee Kinyanjui na Wambora
Gavana Lee Kinyanjui na Wambora
Image: Handout

Magavana wanaoondoka wa Embu na Nakuru Martin Wambora na Lee Kinyajui hawakuonekana katika sherehe za kuapishwa kwa warithi wao Cecily Mbarire na Susan Kihika.

Tofauti na kaunti zingine ambapo watangulizi walikuwepo kukabidhi mamlaka, viti vya hao wawili katika kaunti za Nakuru na Embu vilisalia wazi wakati wa hafla hiyo.

Martin Wambora, Gavana wa Kaunti ya Embu tangu 2013, alishindwa katika azma yake ya kuhudumu kama Seneta katika uchaguzi wa Agosti 9.

Katika kile kilichotajwa kuwa kinyanganyiro kikali, Mundigi aliwashinda Gavana wa Embu Martin Wambora, aliyekuwa wa tano.

Na wagombeaji wengine walikuwa  David Kariuki, Njeru Ndwiga, aliyekuwa kinara Mkuu wa Bunge la Kitaifa Norman Nyagah, na aliyekuwa katibu mkuu Lilian Mbogo Omollo.

Lee Kinyanjui alipata kura 225,623 kwa tikiti ya Jubilee na kushindwa na mgombea wa sasa Susan Kihika, aliyepata kura 440,707 kwa tiketi ya UDA.

Sheria ya kuchukua Ofisi ya Gavana 2019 inamtaka gavana anayeondoka apitishe vipengee vifuatavyo kwa gavana mpya baada ya kutia sahihi cheti cha kuapishwa: bendera ya kaunti, mahakama ya kaunti, katiba na muhuri wa umma.

Hafla ya kuapishwa kwa magavana tofauti hapa nchini ulifanyika mno Agosti 25, ambapo wengi wao na manaibu wao walikula kiapo na kuchukua hatamu ya uongozi kutoka kwa wale magavana wanaondoka