'Hayo ni makubwa,'Hisia tofauti baada ya Sarah na Simon Kabu kupakia picha wakiwa pamoja

Muhtasari
  • Hisia tofauti baada ya Sarah na Simon Kabu kupakia picha wakiwa pamoja
Sarah Kabu na Simon Kabu
Sarah Kabu na Simon Kabu
Image: HISANI

Simon na Sarah Kabu wamekuwa wakivuma mitanddaoni hivi majuzi. Washirika wa biashara walikuwa na shida kubwa katika uhusiano wao.

Sarah alihema moto na alikuwa tayari kuachana na mume wake wa miaka kumi Simon Kabu. Alidai kuwa amekuwa akishughulika na baby mama wa Simon na amechoka sasa.

Pia alitoa ufahamu kwamba alipoolewa na Simon, alijua alikuwa na watoto na wanawake wawili tofauti.

Alikuwa na matumaini kwamba baby mama hao waliotajwa hawataingilia ndoa yao

Simon pia aliongeza chumvi kwenye jeraha baada ya kuondoka na watoto wao kwa siku kumi.

Watoto walikuwa chini ya uangalizi wa Simon na binti yake mkubwa kutoka kwa uhusiano wake wa zamani.

Alikaa mbali na watoto kwa siku kumi na hii ilimkatisha tamaa Sarah sana

Siku ya sikukuu ya pasaka simon Kabu na Sarah Kabu walipakia picha na video wakiwa pamoja  kwenye kurasa zao rasmi za instagram.

Ni jambo ambalo lilizua gumzo mitandaoni na hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki wao;

gigiwaa2: Marriage works, Sarah never let anger takeover. Learn to calm down, never take too it's just a life

kategatune: This is great,, God is great,,,, praying for your family to stay together in Jesus Name

kimani_sophia: Happy to see you together but milly mtoto mdooogo yawa

nicoleshewamb: Please encourage them...they have been there for others too..

madatapaula: Shetani ameshindwa kwa jina la Yesu