Nimechoka kukaa single- Mwanavlogu Kinuthia akiri

Muhtasari
  • Mwanavlogu Kelvin KInuthia kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewaacha mashabiki wake na gumzo baada ya kudai kwama amechoka kuwa Single
Kelvin Kinuthia
Image: Mercy Mumo

Anafahamika sana mitandaoni kwa mavazi yake ya kike, na ucheshii wake ambao amekuwa akifanya kwa muda sasa.

Mwanavlogu Kelvin KInuthia kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewaacha mashabiki wake na gumzo baada ya kudai kwama amechoka kuwa Single.

Kinuthia hajakuwa akipakia uhusiano wake mitandaoni wala kumtambulisha mpenzi wake mitandaoni, baadhi ya wanamitandao wamekuwa wakiuliza jinsia yake kutokana na mavazi yake.

Mwanavlogu huyo amesema kwamba amechoka kuwa single ina maana kuwa anamtafuta mpenzi wa maisha yake.

"ACHA NISEME UKWELI NIMECHOKA KUKAA SINGLE😩💔."

Mapema mwezi jana akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo Kinuthia alizungumzia mambo kadha wa kadha huku akifichua kwamba akiwa na umri wa chini alikuwa anavalia nguo za mama yake.

"Ningependa kuitwa Kinuthia tu, hiyo ni sawa. Mi husema kile mtu atataka kuniita,ni sawa. Mimi niko sawa. Ukiniita mwanamke siweze kuhukumu kwa sababu hata navalia kama mwanamke," Alisema.

Mwavlogu huyo hata hivyo alikataa kuweka wazi jinsia yake halisi ambayo imeendelea kuibua utata mwingi miongoni mwa watumizi wa mitandao ya kijamii.