Marioo akana wapenzi wake wa zamani

Muhtasari

•Mazungumzo haya yalijiri baada ya msanii huyo kutoa ngoma yake mpya 'Dear ex'

•Brandy alidai kuwa sababu kuu ya kutengana na  Marioo, ni kwamba  Marioo alipenda wanawake wengi sana.

Staa wa Bongo Omary Mwanga almaarufu Marioo anayefamika kwa ngoma yake ya 'Mi Amor' aliyeshirikisha Jovial alikana wapenzi wake wa zamani wakati akihojiwa katika kituo moja cha Radio huko Tanzania.

Mazungumzo haya yalijiri baada ya msanii huyo kutoa ngoma yake mpya 'Dear ex'

Katika mahojiano hayo, Mpenzi wake wa zamani anayefahamika kama Brandy,aliwekawazi kwamba mapenzi yao na Marioo yalikuwa ya dhati.

''Omary ni mwanaume ambaye hana maneno mengi akiwa katika mahusiano'' Brandy alisema.

Brandy alidai kuwa sababu kuu ya kutengana na  Marioo, ni kwamba  Marioo alipenda wanawake wengi sana.

''Si unajua msanii alivyo akishapata umaarufa anakutana na kila mtu kwa desigh yake yeye akanisahau'' Brandy alisema.

Wakati huo, Brandy alieleza kuwa Marioo ni mtu mwenye wivu na hataki kuona mpenzi wake na mwanume mwingine.

''Mimi na Bright tulifanya kazi kwa pamoja, kwa mainterview nilikuwa naenda, yeye akiniona na Bright tumeposti anakashirika na kusema vitu mingi'' Brandy alisema.

Aliongeza kwa kusema kuwa sifa moja ya Marioo ni kwamba si mtu ambaye anakashirika kwa haraka.

''Omary ni mtu ambaye  akikashirika hakupigi kwa mkono, lakini kwa maneno,ataongea sana na mwisho wake anatulia, ni mtu ambaye ananuna sana '' Brandy alisema. 

Licha ya Brandy kumsifu Marioo, alikana kwamba hawezi kurudiana na huyo mpenzi wake wa zamani.

Marioo kwa upande wake alikana Brandy na Tunu katika mahojiano hiyo  na kusema kuwa hawajui na hajawai kuwa nao kwenye mahusiano.

''Mimi nawajua ka mashemeji wangu na sijawai kuwa na yeyeto kwenye mahusiano, lakini they are my best friend'' Marioo alisema.