MC Jessy awaita wanawake wanao tumia maji ya bamia "Red Flags"

Jesse alizungumza kuhusu maji ya bamia na kubainisha kuwa huo ni utapeli.

Muhtasari
  • Okra water ni kashfa. Fikiria wewe ni mpango wa kando wa mtu, na huyo mtu wako ako na  bibi, sasa niulize nani anafaa kutumia hiyo maji ya bamia? mpango wa kando ama bibi? Si ni bibi."
MC Jessy
Image: Instagram

Mchekeshaji na mwanasiasa MC Jesse amezungumza kuhusu maji ya bamia yenye imeenea.

Jesse alizungumza kuhusu maji ya bamia na kubainisha kuwa huo ni utapeli. Aliwaonya wanaume dhidi ya kujihusisha na wanawake wanaotumia maji ya bamia.

"Wanadada wameibuka na kusema maji ya bamia yanamfanya mumeo apige kelele usiku, haya maji ya bamia ni utapeli, ni uzushi, ikiwa bibi yako anatumia maji ya bamia au umepata mwanamke anayetumia maji ya bamia,yeye ni 'red flag'. Kwanini anaitumia? Kwani umeshindwa na kazi ndio aitumie?"

Okra water ni kashfa. Fikiria wewe ni mpango wa kando wa mtu, na huyo mtu wako ako na  bibi, sasa niulize nani anafaa kutumia hiyo maji ya bamia? mpango wa kando ama bibi? Si ni bibi."

Mchekeshaji huyo ambaye alikuwa akisafiri hadi Australia, alizungumza pia kuhusu maonyesho yake ya kimataifa.

Jesse alifichua kuwa hakuwa na muda wa kusafiri na kukutana na mashabiki wake wa kimataifa kwani hapo awali alijikita katika siasa.

“Wakenya na Waaustralia wana kitu cha pekee kwao, vichekesho vimekubalika. Namshukuru Mungu kwa sababu brand Jesse imekuwepo kuanzia kitambo. Hatukuwa na muda wa kufanya shoo za  kimataifa. Wamekuwa wakinipiga simu. Niliona kwamba nilikuwa na wakati, kwa hivyo niliamua kutimiza matakwa ya mashabiki wangu, nilikuwa nimeenda kwenye siasa."

Mchekeshaji huyo alifichua kwamba walikuwa na maonyesho ambayo tikiti zote zilikuwa zimeuzwa  nchini Australia, na aliwashukuru mashabiki wake.

"Imepangwa vizuri. Tumechukua waandaaji wakubwa katika kila jiji. Tunaanzia Perth, ambayo imeuzwa kabisa."