Mpenziwe Marioo azungumzia video aliyoonekana akijivinjari na Diamond

Kwenye video hiyo Diamond na Mimi Mars walionekana ndani ya maji wakiwa wamevalia mavazi ya kuogelea

Muhtasari
  • Alikuwa akijibu video ambayo ilisambaa mitandaoni huku yeye na Diamond Platnumz wakiburudika kwenye bwawa la kuogelea

 Mimi Mars dada yake Vanessa Mdee amejibu madai kuwa yeye na Diamond Platnumz wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Alikuwa akijibu video ambayo ilisambaa mitandaoni huku yeye na Diamond Platnumz wakiburudika kwenye bwawa la kuogelea.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Millard Ayo, alisema

"Ilitokea tu kwamba nilikuwa huko kwa mradi wa kazi."

Diamond alithibitisha kumualika Mimi Mars kwenye nyumba yake ya kifahari jijini Dar ambapo wawili hao walionekana wakiburudika kwenye bwawa hilo.

Mwimbaji wa Tanzania, Marioo alifunguka akisema aliumia wakati video ya mpenzi wake, Mimi Mars akiogelea na Diamond Platnumz, ilipoibuka mtandaoni.

Marioo akishirikisha mashabiki wake kwenye kipindi cha maswali na majibu alifichua kuwa hilo ndilo tukio ambalo limewahi kuumiza zaidi maishani.

"Yapo mengi ila nilivoonaga ile klipu video ya rafiki yangu wa kike anaogelea kwenye pool la broo ilinigusa nayo ile," Marioo alimjibu shabiki aliyeuliza kuhusu tukio ambalo limewahi kumuumiza zaidi.

Kwenye video hiyo Diamond na Mimi Mars walionekana ndani ya maji wakiwa wamevalia mavazi ya kuogelea huku  wakijivinjari na kucheka.