Apakia picha ya zamani na ya sasa, asema mpenzi wake alimuacha kwa kuwa na sura mbaya

Hatuo sawa katika fadhila - Dorothy aliandika.

Muhtasari

• “Aliniacha kwa sababu nilikuwa sipendezi, niko kama tomboy na mwenye kelele nyingi, ila bado ni mwenye kelele nyingi hata kama,” Dorothy Cornelius aliandika

Alisema aliachwa juu ya kutopendeza na mpenzi wake.
Dorothy Cornelius Alisema aliachwa juu ya kutopendeza na mpenzi wake.
Image: Tiktok

Mwanamke mmoja kwa jina Dorothy Cornelius amewaacha watumizi wa mtandao wa TikTok wakizungumza baada ya kuunda video moja ambapo alipakia picha yake ya zamani na ya sasa huku akidokeza kwamba aliyekuwa mpenzi wake alimuacha kwa visingizio vya kuwa duni mwenye sura mbaya.

Katika video hiyo yenye picha mbili; ya zamani na ya sasa, Dorothy anaandika kwa hiyo ya zamani kwamba mpeniz wake alimbwaga kwqa sababu za kuwa na sura isiyo ya kuvutia na ambayo inakaa kama mdoli wa kiume na kelele nyingi.

Kwenye picha ya pili ambayo ina utofauti mkubwa kutokana na ustawi wa Ngozi yake iliyonadhifishwa kwa urembo maridhawa, Dorothy anadokeza kwamba licha ya kubadilika na kuongeza urembo ila bado suala la kelele bado lipo pale pale kwani ni tabia yake na kwa kuwa tabia ni Ngozi basi inakuwa vigumu kuitenganisha na mtu husika.

“Aliniacha kwa sababu nilikuwa sipendezi, niko kama tomboy na mwenye kelele nyingi, ila bado ni mwenye kelele nyingi hata kama,” Dorothy Cornelius aliandika kwenye klipu hiyo fupi ambayo imesambazwa sana na kuona na watu takribani laki nane.

Ama kweli maisha ni safari ndefu sana isiyo na likizo, na ambaye ataivumilia katika yote jana yake haiwezi kuwa sawa na kesho yake!