Kwa nini Harmonize alikosa kwenye orodha ya Forbes, Diamond na Rayvanny wakitajwa?

Diamond na Rayvanny ndio wasanii pekee kutoka Afrika mashariki waliotajwa kwenye orodha ya Forbes ya wasanii 20 bora Afrika.

Muhtasari

• Rayvanny amefanya makubwa sana hivi karibuni hivyo ni sahihi kabisa kuingia katika list hiyo.

• Huwezi kulizungumzia soko la bongo fleva pasi na kumtaja Diamond ndani na nje ya Afrika mashariki tena kwenye kurasa kadhaa.

Wasanii wa bongo fleva, Harmonize, Diamond Platnumz na Rayvanny
Wasanii wa bongo fleva, Harmonize, Diamond Platnumz na Rayvanny
Image: Instagram, YouTube screengrab

Wiki iliyopita jariba la kuthathmini ubora wa watu katika sekta mbali mbali maishani, haswa kwa kuzingatia utajiri, Forbes liliachia orodha ya wasanii wenye nguvu zaidi barani Afrika na katika orodha hiyo kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, tumewakilishwa na msanii Diamond Platnumz na mwenzake Rayvanny.

Wasanii hawa wawili wamefanya mambo makubwa katika siku za hivi karibuni ikiwemo kuvunja rekodi mbalimbali na ndio wamekuwa wa kwanza kabisa kutoka ukanda huu kuingia katika orodha ya Forbes ya wasanii bora katika udongo wa Afrika.

Orodha hiyo imewajumuisha wengi wa wasanii kutoka Nigeria ambao kwa kweli bila nongwa wamekuwa wakilibeba bara hili katika majukwaa mbali mbali ulimwenguni na kuwepo pale ni haki na stahili.

Diamond na Rayvanny wana jivunia kuwepo kwenye orodha hiyo pamoja na majina makubwa kama Yvonne Chaka Chaka kutoka Afrika Kusini, Wizkid, Burnaboy, Tiwa Savage, Davido Angelique Kijo, Fally Ipupa, Black Coffee, Mr Eazi, Master Kg Casper Nyovest, 2face Idibia, Major League, NastyC, Lira, DJ Maphorisa, Kddo na LeboM. Hii ikiwa ni orodha ya mseto ambayo haijapangwa kulingana na ni nani aliye juu na ni nani anayefuata.

Wengi haswa mashabiki wa muziki Tanzania walikuwa wanategemea kwamba jina la msanii Hamronize lingekuwepo kwenye orodha hiyo haswa baada ya kitajwa kufanya vizuri il ani butwaa kwa mashabiki wake na hili limezua mjadala mkali miongoni mwa wadau wa muziki nchini humo, baadhi wakihisi Harmonize alidhulumiwa na nafasi yake kupewa Rayvanny huku wengine wakihisi Rayvanny alistahiki baada ya kuvunja rekodi kadhaa hivi karibuni.

“Katika hali ya uhalisia tu, Harmonize hastahili kwa sasa kuingia katika orodha hiyo maana bado muziki wake umejikita sana ndani ya Tanzania na Afrika mashariki kwa mbali. Rayvanny amefanya makubwa sana hivi karibuni hivyo ni sahihi kabisa kuingia katika list hiyo, Diamond Pia hawezi kukosa katika List hii, Balaa lake mnalifahamu,” mdau mmoja alitolea maoni.

Wengine walizua kwa kusema kwamab Harmonize kukosa ni kawaida tu kwani mbona hata Alikiba amekosa kweney orodha hiyo na hakuna minong’ono?