H-Baba amchana Mwijaku kwa kuingilia mambo ya ndani ya Harmonize na bintiye Paula

Vile vile alisema kuwa msanii Diamond aliacha kitambo kupokea simu za Mwijaku.

Muhtasari

• H Baba alimsuta Mwijaku kwa tabia ya kuingia kwenye masebule ya watu na kuanza kutoa mambo ya ndani mwa watu kuyaweka wazi kwa umma.

H Baba amwambia Mwijaku kukoma kuingilia mambo ya Harmoniz\e ya ndani
H Baba amwambia Mwijaku kukoma kuingilia mambo ya Harmoniz\e ya ndani
Image: InstaGRAM

Msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva ambaye hivi karibuni ameonekana kuwa kibaraka wa Diamond, H Baba amefichua kwamba mkurugenzi huyo mkuu wa WCB Wasafi hapokei simu za mtangazaji mchonganishi Mwijaku.

Kwa mara ya kwanza, H Baba ambaye amekuwa akidhihirisha tofauti zake wazi wazi na Harmonize alimtetea safari hii dhidi ya matamshi ya Mwijaku kwamba aliingia katika sebule yake na kumkuta binti Paula Kajala akimkanda kifuani.

H Baba alimsuta Mwijaku kwa tabia ya kuingia kwenye masebule ya watu na kuanza kutoa mambo ya ndani mwa watu kuyaweka wazi kwa umma.

Vile vile alisema kwamba katika hilo anamtetea Harmonize kwa vile mambo ambayo wanafaa kuchafuana ni ya nje tu wala ya ndani yabaki kuwa siri za watu wahusika wenyewe.

Alikanusha madai kwamba huenda Mwijaku ametumwa na Diamond ili kumchafulia jina Harmonize na kusema kwamba ikiwa ana namba ya Simba basi hajawahi zungumza na yeye moja kwa moja na kudai kuwa Mwijaku atabakia katika njia kuu ya kuwa balozi wa Wasafi Bet.

“Diamond hana muda mchafu na mimi nasema leo, kama ana namba ya Diamond, anayo sawa, lakini Diamond hapokei simu ya Mwijaku na hajawahi pokea simu yake. Mwijaku anaonana na watu wa chini tu wala hawezi kuonana na Simba. Wanakutana tu kwenye shoo,” H Baba alisema.