Jumbe za wanamuziki wa nchi zingine kwa Davido na Chioma

Watu wengi maarufu wamewatumia Davido na Chioma jumbe za kuwafariji.

Muhtasari

• Mwanamuziki mashuhuri wa Trinidad, Nicki Minaj alitumia familia ya Davido rambirambi na kuwatakia mema baada ya mtoto wao kufariki.

Nicki Minaj, Wizkid na Stefflondon

Inadaiwa kuwa mtoto wa mwanamuziki wa Nigeria Davido, Ifeanyi Adeleke alifariki kwa kuzama alipokuwa anaogelea  katika bwawa la nyumbani

Davido na mchumba wake Chioma walikuwa wameenda kwenye mtoko na kuwaacha walezi kumwangalia mwanao.

Baadhi ya wanamuziki maarufu wameandika ujumbe wa rambirambi kwa wapenzi hao.

Nicki Minaj

Mwanamuziki mashuhuri wa Trinidad alitumia familia ya Davido rambirambi na kuwatakia mema baada ya mtoto wao kufariki.

"Natuma rambirambi zangu kwa Chioma na Davido," aliandika.

Wizkid

Mwanamuziki huyo alifuta ujumbe uliotangaza siku atakayozindua albamu yake ya 'More Love, Less Ego' na kuahirisha siku yake ya uzinduzi kama heshima kwa mtoto wa Davido.

Ruger

Ruger alihuzunika baada ya wanamitandao kuendelea na maisha yao baada ya siku mbili za kufahamu kuwa Davido alimpoteza mwanawe.

"Dunia na kila kitu haimaanishi lolote, maanake kila mtu amerudi kupakia picha zao nzuri na machapisho katika kurasa zao baada ya muda mfupi tu wa kuandika 'Mungu Kwa nini'. Sisi binadamu ni giza na utupu ambao unafaa kuuhamishwa kutoka ulimwengu huu mzuri kwa sababu ulimwengu huu bado ungekuwa mzuri bila sisi," Ruger aliandika.

Stefflon Don

Rapa huyo alituma rambirambi zake za kuwatakia mema Davido na Chioma katika ukurasa wake wa Twitter.

"Waombeeni Davido na Chioma," alisema.

Meek Mill

"Maombi kwa Davido na familia yake. Nawaombea wote," aliandika huko Twitter.

Bobi wine

"Natuma rambirambi za dhati kabisa kwa Davido na mke wako kwa kufiwa na mtoto wenu. Mungu awape nguvu ya kujikakamua kwa wakati huu mgumu," alisema.