Wahu aelezea taabu za kulea mtoto mchanga, "Nimeimba mpaka za Celine Dion lakini wapi!"

Lakini kwa nini Mungu hakupanga tu watoto kulala usiku kutoka siku ya kwanza? - Wahu aliuliza.

Muhtasari

• Watumizi wa mitandao walimpa ushauri jinsi ya kuhakikisha mtoto analala huku wengine wakimtaka kuendelea kuimba akizunguka naye chumbani.

Mabinti wa Nameless; Tumiso, Nyakio na Shiru.
Image: FACEBOOK// NAMELESS

Manamuziki wa muda wote nchini Kenya, Wahu Kagwi ambaye pia ni mama mpya mjini amesimulia masaibu ya kulea mtoto mdogo.

Wahu ambaye mapema mwezi Oktoba alibarikiwa na mtoto wake wa tatu, binti alipakia majira ya usku mkuu kuamkia Desemba 6 na kusimulia kuwa usiku huo ulikuwa na changamoto za aina yake kutoka kwa bintiye mchanga, Shiru.

Alisema kuwa alijaribu kumuimbia bembelezi za kila aina mpaka zile ambazo zimetungwa na msanii wa kimataifa, Celine Dion lakini zote ziliangukia kwenye maskio ya kiziwi kwani mwanwe alizidi kulia usiku wote.

“Leo nimeimba mpaka za Celine Dion, lakini wapi. Lakini kwa nini Mungu hakupanga tu watoto kulala usiku kutoka siku ya kwanza?” Wahu aliandika huku akidokeza kuwa si wote wanaweza kumuelewa bali wale tu ambao wamepitia moto kama huo kipindi cha nyuma.

Wahu aliongeza zamu ya hashtag usiku akimaanisha kuwa aliwekwa macho na mtoto.

Watumizi wa mtandao wa Facebook ambako aliandika ujumbe huu walijumuika naye usiku huo na kumpa shavu huku wakimtia moyo kuwa hali hiyo haitadumu milele kwani Shiru anakua na punde si punde atakuja kusimulia jinsi alikuwa anamkosesha usingizi usiku wote.

“Shiru anataka uanze kumuombea kwa msingi wake mzuri, omba, zunguka kwa nyumba ukiomba na kumtakia mazuri na utashtukia amelala hata kabla umalize,” mmoja alisema.

“Ninakumbuka wakati huo pia mimi mapacha wangu walikuwa wanalia name nalia pia,” mwingine alisimulia jinsi changamoto zake zilikuwa enzi akiwa na watoto wachanga.